Social Icons

Jumatatu, 8 Septemba 2014

Je, Hizi ni Siku Za Mwisho?


Nabii Daniel alizungumza juu ya “WAKATI WA MWISHO.” Mtume Petro alisema, “katika SIKU ZA MWISHO watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki.” Paulo alisema, “SIKU ZA MWISHO kutakuwako nyakati za hatari.” Wanafunzi wa Kristo walimwuliza juu ya “MWISHO WA ULIMWENGU.” Je, wakati huo umefika? Unaweza kuwa na uhakika?

Mpaka lini Kristo atarudi? Kabla tukio hili kubwa kuliko yote halijatokea, Biblia huongelea juu ya kipindi kinachoitwa “siku za mwisho”—“wakati wa mwisho”—­“mwisho wa ulimwengu [zama]”—“mwisho wa mambo haya”—“mwisho wa siku”—na ya wakati ambapo historia ya mwanadamu, kama tuijuavyo, “itakapomalizika.”
Bila shaka, wengi wanaojidai kuwa Wakristo hawaamini katika tukio halisi la kurudi kwa Yesu Kristo duniani. Miongoni mwa wanaoamini, wengi wao huamini kwamba inaweza kutokea baada ya miaka mamia ijayo. Baadhi wanaamini inaweza kuwa “miaka maelfu ijayo.” Wengine kwa namna fulani wanafikiria juu ya “Har-Magedoni.” Wanahisi kwamba wakati unaweza kuwa mfupi lakini hawana uwezo wa namna ya KUJUA.
Wewe unaamini nini?

Mitume wa Awali Walielewa Isivyo

Mitume wa awali walifikiri kwamba Kristo angerudi wakati wa maisha yao. Paulo katika 1 Wakorintho 15:51 na 1 Wathesalonike 4:15, alipokuwa akiongelea ufufuo wa wafu utakaotokea Kristo anaporudi mara ya pili, alitumia neno “sisi” akitegemea kuwa mmoja wa wale ambao wangekuwa “hai, [tutakao] salia hata wakati wa kuja kwake Bwana.”
Katika waraka wake wa pili kwa Wathesalonike, Paulo alikuwa amegundua kwamba hapo awali alikuwa ameelewa vibaya muda wa kutokea matukio maalumu ambayo ni lazima yatangulie Kurudi kwa Kristo. Alienda mbele na kuonya dhidi ya wale ambao wangedanganya wengine juu ya lini tukio hili lingetokea. Aliandika juu ya “kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo” na ndugu wanapaswa wawe waangalifu kwamba “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu” (2 Wathesalonike 2:1, 3).
Je, unaweza kudanganyika?

Kurudi kwa Kristo Mara ya Pili

Je, tuko kwenye siku za mwisho? Kama ndivyo, unaweza kujua kwa hakika kwamba hii ni kweli? Yesu alisema kwa wanafunzi wake, “Nitarudi tena” (Yohana 14:3). Siku arobaini baada ya kufufuka kwake, wanaume wawili (malaika) waliwaambia wanafunzi wake wakati anapaa mbinguni, “Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni” (Matendo 1:11). Mathayo anaandika maneno ya Kristo: “Maana kama vile umeme uonekanavyo…ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu” (Math. 24:27, 30, 37, 39, 42, 44, 46). Je, karibu ulimwengu utalifikia tukio hili la upeo wa juu kabisa? Tena, je, tunaweza kujua?
Usifanye kosa! Biblia iko wazi kuhusu Kurudi kwa Yesu Kristo. Mafungu mengi zaidi yanayoongelea Kurudi Kwake Mara ya Pili duniani yanaweza kunukuliwa. Kutatokea—na haitegemei juu ya mapendekezo ya wanadamu. Hata hivyo, kabla tukio hili la juu kabisa halijatokea, mambo mengine mengi zaidi yalisemwa yatatokea katika kipindi cha kuelekea matukio ya kutisha yanayotangulia kurudi kwake!
Dhana ya mwisho wa ulimwengu limekuwa ni somo lenye hisia, kejeli, mjadala, kusisimua na linalowafanya watu wafikiri kwa miaka 2,000. Bado, ni wachache wanaofahamu kiasi gani Biblia inaonyesha juu ya kile kinachoweza kueleweka kuhusu wakati huu.

“Siku na Saa”

Katika unabii maarufu wa Mlima wa Mizeituni kwenye Mathayo 24, wanafunzi walimwuliza Kristo, “Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja Kwako, na ya mwisho wa dunia?” (fu. 3). Baada ya kujibu swali hili kwa kirefu, mafungu thelethini-na-tatu baadaye Kristo aliongeza, “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake” (fu. 36).
Je, hii inamaanisha kwamba hatuwezi kujua kiujumla wakati wa Kuja kwa Yesu Mara ya Pili? Baadhi wanaamini hivi—na watu hawa hutupilia mbali hitaji lolote la kujishughulisha ili kujua lini kutakuwa Kurudi kwa Kristo.
Mathayo 24:50-51 humaanisha nini inaposema, “bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki”? Ni wazi kwamba karibu kila mmoja hategemei Kurudi kwa Kristo Mara ya Pili katika wakati sahihi. Ukweli ni kwamba atarudi wakati ambapo wengi hawamtazamii kabisa. Kitu gani kitawafanya wengi wasitambue mwanzo wa tukio hili kubwa?
Kwa nini kuna wengi sana ambao hawawezi kutambua kuwasili kwa siku za mwisho?
Katika mafungu ya 32-33, Kristo alitoa mfano: “Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu; nanyi kadhalika,myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.” Kristo alitamka kuwa tunaweza kujuamajira” ya Kurudi kwake Mara ya Pili,
Usiwe tayari kuridhika bila kujua kile ambacho Biblia inasema unaweza kujua!
Miaka mingi iliyopita, kulikuwa na usemi maarufu uliojulikana kama “Ishara za Nyakati”. Niliufurahia na pengine nawe unaukumbuka. Kichwa hicho kilitolewa kwenye fungu lingine katika Mathayo. Kwenye sura ya 16, Mafarisayo na Masadukayo walimkabili Kristo, wakitaka “ishara” kutoka kwake. Aliwaita wanafiki, akisema, “Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa mbingu; lakini, je! Ishara za zamani hizi hamwezi kuzitambua?
Ingawa lengo la swali lao lilikuwa kutaka ishara kwamba Yesu alikuwa MASIHI (angalia Mathayo 12:38-40), mantiki ya Kristo ilikuwa kwamba hawakuweza kutambua matukio waliyokuwa wakiyashuhudia—“ishara za nyakati.”
Je, unaweza kutambua ishara za nyakazi ZETU?
Kristo aliwaambia wanafunzi wake, “Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia” (Luka 21:28). “Mambo” ambayo aliyarejelea yanajumuisha mfululizo mzima wa matukio yaliyotabiriwa kutokea kwa mara ya kwanza katika historia! Mambo hayayanatokea—na yanazidi—sasa! Kuyatazama kwa haraka haraka hakutasaidia. Ni lazima tuchunguze kwa umakini ili kuweza kuzitambua “ishara za nyakati.”
Mungu amemtengea mwanadamu miaka 6,000 kujaribu serikali zake mwenyewe, falisafa, mifumo ya maadili, dini na miundo ya elimu. Fikira za kibinadamu hazitatui na hazina uwezo wa kumaliza matatizo makubwa ya ulimwengu. Miaka 6,000 ni kama imemalizika. Na, katika miaka 200 iliyopita au zaidi, ulimwengu umebadilika sana—na kwa haraka. Matukio yanatokea kwa haraka kwa namna ambayo haijawahi kuonekana huko nyuma!

Ulimwengu wa Karne ya Ishirini-na-moja

Kila mmoja anawafahamu watu fulani ambao huzunguka zunguka wakisimama kwenye mitaa wakipaaza sauti “Tubuni! Mwisho umekaribia!” Kikundi cha filamu cha Holywood kimewaigiza wengi kati yao. Bila shaka, hakuna mtu anayewajali sana watu kama hao. Lakini nyakati zimebadilika, na sauti zinazotuambia sasa kuwa mambo hayaendi sawa zimekuwa nyingi—tena mambo ni mabaya kabisa!
Wazo la kuwa na serikali moja ya dunia, lilibuniwa ili kuiokoa sayari na mwanadamu asijiangamize, linasikika mara nyingi zaidi. Hata hivyo, hakuna anayeonekana kujua namna ya kuunda serikali kama hiyo na kisha kupata ushirikiano wa kila mmoja ulio wa lazima ili kuifanya ifanikiwe!
Utazame ulimwengu unaokuzunguka. Unaona nini?
Ulimwengu mzima ulikuwa ni mahali imara mpaka mwanzoni mwa karne ya kumi-na-tisa. Katika wakati huo maendeleo ya viwanda yalizaa Zama Mpya. Haikuwahi kutokea mpaka takribani karne moja iliyopita ambapo watu walianza kuendesha magari na kuruka kwa ndege, na, tangu wakati huo, ustaarabu umekwenda kutoka “Zama za Nyukilia” hadi “Zama za Anga” na ndani ya muda mfupi chini ya nusu karne umefikia “Zama za Habari”.
Kuwasili kwa mavumbuzi mapya, kwa kasi kubwa katika historia, inabadilisha maisha kila siku. Hebu fikiria matokeo ya viwanda vya uchapaji na utaweza kukubali namna ambavyo uvumbuzi wa aina moja unavyoweza kuubadilisha ulimwengu. Kompyuta za kisasa zimefanya yayo hayo—na hakuna kurudi nyuma kwa sababu tu ya uvumbuzi huu mkubwa. Usafiri wa ndege uliwasili mwishoni mwa karne iliyopita. Japokuwa makadirio yanatofautiana lakini inasemekana kwamba maarifa ya mwanadamu yanaongezeka mara dufu kila baada ya miaka michache. Baadhi wanafikiri kuwa baada ya muda mfupi kasi itaserereka hadi kufikia kila baada ya miezi sita!
Mnamo mwanzoni mwa miaka ya 1970, Alvin Toffler aliandika kitabu kinachoitwa Fadhaa Ijayo (Future Shock). Kitabu hiki kikubwa kilielezea aina ya “bumbuwazi la kisaikolojia,” au madhara ya fadhaa, yatakayowapata watu kwa sababu ya kasi ya mabadiliko katika jamii. Toffler alidhihirisha kuwa mabadiliko haya yalianza kutokea miaka ya 1970 katika kiwango ambacho watu hawakuweza tena kuyatafakari. Jamii ilianza kuingia kwenye kile ambacho Toffler alikielezea kama kuzidiwa—au “fadhaa.” Alielezea kwamba “yajayo” yalikuwa yanakuwa “yaliyopo” kwa haraka sana kiasi kwamba watu walianza “kutumia njia za mkato” namna ile ambayo ustaarabu ulikuwa haujawahi kuona. Miaka michache baadaye, aliandika kitabu kinachofutia kile cha kwanza kilichoitwa Wimbi la Tatu (The Third Wave). Kitabu hiki cha pili kilielezea kuongezeka kwa hali hii.
Picha aliyoielezea haikuwa nzuri, na sasa imekuwa mbaya zaidi!
Wakati “maendeleo” haya makubwa yakitokea, matatizo ya mwanadamu yamezidi kuwa makubwa auyasiyotatulika zaidi!
Makadirio ya ukubwa wa tatizo la UKIMWI yanapitiwa upya mara kwa mara na kuakisi mtazamo unaotisha zaidi kuliko ilivyofikiriwa hapo kabla. Sehemu nzima za wakazi wa Afrika zinakadiriwa kufutika kabisa ndani ya miaka michache kwa sababu tu ya ugonjwa huu mmoja.
Idadi ya watu duniani inayokadiriwa kuwa bilioni 6.9 (mapema 2009) inaongezeka kwa kiwango cha 1.2% kila mwaka. Hii ina maana kwamba kufikia mwaka 2050, idadi ya watu duniani itafikia bilioni 11.1! Makadirio haya yanakuja ingawa kuna ukweli kwamba magonjwa na njaa vinategemewa kuongezeka zaidi kwenye sehemu za dunia zinazokua kwa haraka sana! Kuzaliana kwa wingi katika nchi maskini duniani tayari kumeleta ongezeko hili la watu kama ilivyokadiriwa kutokea.

Unabii wa Siku za Mwisho

Hebu tuchunguze baadhi ya aya za Biblia zinazoelezea unabii madhubuti kuhusu mwisho wa wakati!
Tumekwisha kuelezea kuwa Paulo alikuja kugundua kuwa hakuishi kipindi ambacho Kristo angerudi. Hata hivyo, Mungu alimtumia kuandika namna hali itakavyokuwa mara wakati huo utakapowadia. Zingatia unabii wake juu ya kuenea kwa mmomonyoko wa maadili na tabia, kipindi kifupi kabla ya Kurudi kwa Kristo Mara ya Pili. Aliandika, “Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao” (2 Tim. 3:1-6).
Huu ni unabii mzito unaoelezea kuharibika kabisa kwa tabia katika “siku za mwisho.” Wakati huu umefika!—na hali hii iliyoenea duniani kote inaendelea kuwa mbaya zaidi kila siku! Angalia mahali ulipo. Tabia za watu zinabadilika kwa kasi kubwa—wakati wote zinazidi kuwa mbaya. Waelimishaji na wengine walioko madarakani wanapaaza sauti kuwa hali imelipuka kufikia kiwango kisichoweza kuthibitiwa!
Nani anaweza kutilia shaka hali hii?
Tambua kuwa kijitabu hiki hakijaandika kwa kirefu. Ingekuwa hivyo, kurasa nyingi zingehitajika kuelezea hali ile ambayo Paulo aliirejelea katika unabii huu mmoja!
Lakini kuvunjika kwa maadili na mienendo ya watu kunatofautiana sana kukilinganishwa na kizazi kilichopita. Wakati wote kumekuwa na machafuko ya kutisha lakini sasa yanatokea mara kwa mara. Wakati wote kumekuweko na waongo lakini sasa hali ya uongo imeenea sana. Uzinzi umekuwepo wakati wote lakini asilimia ya watu wanaofanya uzinzi sasa imepindukia. Kumekuwepo na talaka wakati wote lakini sasa imekuwa ni jambo la kawaida sana. Siku zote kumekuwa na vijana wasio na adabu. Si mbali kizazi kizima kitakuwa kimesahau Amri ya Tano, “Waheshimu baba na mama yako.” Ingawa kumekuwa na wizi wakati wote, takwimu zinaonyesha kuwa wizi umepita kiwango—hata kwenye nchi zilizo na mafanikio makubwa kiuchumi, mahali ambapo watu wake wana mali nyingi kwa sababu tu ya mahali pale walipozaliwa!
Kuna mengi zaidi ambayo yanaweza kusemwa juu ya kila neno au usemi katika unabii wa Paulo. Na hatujaongelea juu ya ponografia (picha au maandishi yenye kutia ashiki), uzalilishaji wa watoto, makosa ya jinai na mwelekeo wa mahusiano ya kingono yasiyo ya asili, madawa ya kulevya, chuki na vita! Mambo haya yote yamejumuika pamoja na kuleta kile kinachoelezewa kama “hatari”—au hatari sana! Kwa pamoja, hiki kinakuwa ni kiashiria kwamba hizi ni siku za mwisho!

Unabii Mkuu wa Kristo Katika Mlima wa Mizeituni

Vikiwekwa pamoja, Mathayo 24, Luka 21 na Marko 13 hujumuisha unabii wa Kristo katika Mlima wa Mizeituni. Habari hii inaanza na wanafunzi wake (Math. 24:3) wakimwuliza kuhusu matukio ambayo yangetangulia “mwisho wa ulimwengu.” Wakati huu kilichoulizwa kilikuwa ni “ishara” ya lini mwisho wa zama—mwisho wa jamii iliyostaarabika kama tuijuavyo—utakuja. Kama ilivyotajwa, wanafunzi wake waliamini kuwa hii ingetokea wakati wa maisha yao, kwa sababu waliuona mwisho sambamba na kuangamizwa kwa hekalu la Yerusalemu. Hii ni kwa sababu Kristo alikuwa amemaliza kuelezea wakati huu wa uharibifu uliokuwa unakuja kabla hawajamwuliza swali lao. Wakati hekalu hili liliteketezwa na Warumi katika mwaka wa 70 BK, Kristo alielewa kwamba Kuja Kwake Mara ya Pili kungetokea takribani karne 20 baadaye. Alitabiri kwamba matukio fulani mengine yatatangulia.
Kristo alielezea kuporomoka kwa tabia sawa sawa kama Paulo alivyofanya. Katika mafungu ya 36-39, Kristo alionya kwamba hali itakuwa sawa na “siku za Nuhu,” ambazo Mwanzo 6:11-12 inazielezea: “Duniaikaharibika mbele za Mungu, dunia ikajaa dhuluma. Mungu akaiona dunia, na tazama, imeharibika; maana kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani.”
Uharibifu umetajwa mara tatu katika maelezo haya mafupi. Bado, aya hii ni ya kipekee na inazungumzia watu kwamba, kila mmoja, na kwa pamoja wameporomoka na kufikia hali ya uharibifu mkamilifu—huku ustaarabu “ukijawa na dhuluma.” Angalia Mungu anavyotumia maneno ya umoja “yake” na neno la wingi “wote” kufikisha ujumbe huu!
Fikiria ni mara nyingi kiasi gani vitendo vya dhuluma ya halaiki inavyotokea mashuleni, kwenye migahawa, au maeneo mengine sasa kwa namna ambayo haikuwahi kusikika mpaka hivi karibuni! Nani aliyewahi kusikia wauaji wa kuvizia—au walipuaji wa kujitoa mhanga—kabla ya hivi karibuni? Na hata dhana ya hivi karibuni ya ughaidi sasa imesambaa katika dunia nzima. Hali hii ilitabiriwa kuenea katika ulimwengu mzima.
Katika Luka 17:26-30, Kristo pia alilinganisha hali itakavyokuwa wakati wa Kurudi Kwake na ile iliyokuwa katika miji ya Sodoma na Gomora. Mwanzo 18 na 19 huonyesha kwamba miji hii miwili ilikuwa imeoza na kujaa uovu kiasi kwamba, kabla Mungu hajanyesha moto na kiberiti juu yake, watu watatu tu (Lutu na binti zake wawili—mke wake akibadilika kuwa chumvi baadaye) walihesabiwa kustahili kuepuka. Pia, ni watu wanane tu waliruhusiwa kuingia safinani kabla Mungu hajagharikisha na kuuangamiza ulimwengu.
Jiulize mwenyewe: Itachukua muda gani kabla hali haijawa mbaya zaidi?
Vipi kuhusu mkanganyiko wa kidini? Mathayo 24:4-5 ina kumbukumbu ya onyo la Yesu juu ya udanganyifumkuu unaokuja. Alisema, “Angalieni, mtu asiwadanganye. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi [Yesu] ni Kristo; nao watadanganya wengi.” Kwa maneno mengine, wengi watadaikumwakilisha Yesu, na kukiri kwamba Kristo kweli alikuwa Kristo, wakati wakileta ujumbe ambaohuwadanganya wasikilizaji wao. Makundi mengi ndani ya Ukristo ambayo leo hii, yamegawanyika, kukanganyikiwa, hayakubaliani na yanayoshindana, kwa hakika huthibitisha usahihi wa unabii wa Kristo.
Ni jambo nyeti kuangalia upande mwingine wa onyo la Yesu juu ya wale ambao wangesema, “Kristo alikuwa Kristo.” Karibu wahubiri wote wa kisasa husisitiza zaidi habari za Yesu Mwenyewe, badala yaujumbe aliouleta! Wanalenga zaidi kwa Mjumbe badala ya ujumbe wake! Wakisema kwamba kwa hakika Kristo alikuwa Kristo—Masihi—ni kauli ya kweli! Udanganyifu wa “wengi” unaanza pale ujumbe wake wa ufalme utawalao-ulimwengu, pamoja na kile ambacho tukio hili kuu linamaanisha, hupuuzwa—na hata kuhafifishwa. Hapa ndipo ulipolala udanganyifu mkuu! Elewa hili!
Hebu tuwe bayana zaidi.

Injili ya Uongo Hutangazwa

Yesu alitangaza injili ya ufalme wa Mungu. Marko 1:14-15 huandika haya kama maneno ya kwanza aliyozungumza: “Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu [injili ya ufalme wa Mungu], akisema…ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.” Mafungu mengi katika Agano Jipya huonyesha kuwa daima Kristo alihubiri ujumbe huu. (Soma Kijitabu chetu Injili ya Kweli ni Ipi? na Ufalme wa Mungu ni Nini?)
Miaka thelathini baada ya Yesu kusulubishwa Paulo alionya dhidi ya wale ambao tayari walikuwa wanaipotosha injili na kuifanya iwe tofauti, ya uongo, injili bandia (Gal. 1:6-7). Ufahamu huu ulikuwa wa muhimu sana kiasi kwamba mara mbili alitamka laana kwa yeyote aliyefanya hivi (fu. 8-9). Vile vile alionya, “Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi [urahisi ulio] kwa Kristo. Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingineambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye” (2 Kor. 11:3-4).
Paulo aliwashutumu watumishi wa uongo ambao walileta uongo huo aliposema “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwawatumishi wake [Shetani] nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao” (fu. 13-15). Fungu hili linadhihirisha nguvu ya udanganyifu waliyo nayo “wengi” (ambao Kristo aliwarejelea katika Mathayo 24)—watumishi wengi wa Ukristo wa dunia hii. Kwa wazi huongelea wahubiri ambao humwakilisha Kristo isivyo kwa Kuhubiri “Yesu mwingine” na kuleta “injili nyingine,” tofauti na ile ya ufalme wa Mungu.
Mara nyingi Paulo ameelezewa kwamba alileta injili nyingine. Bado, imeandikwa kwamba yeye pia alihubiri ufalme wa Mungu (Matendo 20:25; 28:23-31).
Watumishi wa makanisa ya ulimwengu huu hawahubiri ujumbe huu! Wanahubiri mfululizo juu ya “mtoto Yesu,” “Kristo msalabani,” “bikra kuzaa mtoto” na injili mbali mbali za kijamii. Lakini ni mara ngapi umesikia kwamba Kristo anakuja kutawala dunia kama Mfalme—akileta SERIKALI BORA iliyo kuu itakayoziondoa na kuchukua mahali pa serikali zote za wanadamu? Pengine kamwe hujawahi.

Pengo la Miaka 1,900

Mpaka hapo Herbert W. Armstrong alipoanza kuitangaza injili hii kwa ulimwengu katika mwaka 1934, injili ya ufalme wa Mungu ilikuwa haijawahi kupelekwa kwa mataifa yote kwa takribani miaka 1,900. Tangu siku za mitume, mpaka kuanza kwa huduma ya miaka 52 ya mtu huyu, injili ya kweli haikuenea kwa nguvu ulimwengu kote!
Mathayo 24:14, na sehemu ya Unabii wa Mlima wa Mizeituni, husema, “Tena habari njema ya ufalmeitahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” Bwana Armstrong aliwafikia mamia ya mamilioni wakati wa huduma yake. Hii ni pamoja na wasomaji wa gazeti la Ukweli Dhahiri [Plain Truth] wapatao milioni 25 (zaidi ya familia milioni 8 zilizojisajili kutumiwa gazeti hilo) walikuwa wamefikiwa mpaka alipofariki, mwanzoni mwa mwaka 1986. Gazeti hili lilichapishwa katika lugha saba! Bwana Armstrong mwenyewe aliwatembelea moja-ya-tatu ya wakuu wa nchi duniani katika miongo miwili ya mwisho wa maisha yake. Muda wote alileta ujumbe huu huu wa ufalme wa Mungu ujao.
Kuna maeneo machache duniani ambapo ujumbe huu haukusikiwa ama kwenye redio au runinga. Ujumbe huu ulitangazwa kwenye mamilioni ya vituo. Wakati fulani matangazo yake ya Ulimwengu wa Kesho [Word Tomorrow] yalipata kuwa ndiyo matangazo ya kidini yaliyosikilizwa zaidi duniani kulingana na ulinganishaji wa Arbitron. Injili ya ufalme ilienda kwa nguvu kubwa—kuliko wakati wowote katika historia!
Unabii wa Kristo ulikuwa, na bado ni, kweli!

Vita, Njaa, Ndwele na Matetemeko

Uangalie vizuri ulimwengu unaokuzunguka! Ni wazi kwamba hauongozwi na Mungu, badala yake umejaa matatizo, maovu, maumivu, majanga na huzuni za kila namna. Kristo alionya, “Nanyi mtasikia habari zavita na matetesi ya vita…kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali” (Math. 24:6-7). Aliendelea kusema kwenye fungu la 8, “Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu [majaribu].” Pia aliwaambia wanafunzi kwamba watateswa vibaya hata kuuawa kwa ajili ya ujumbe watakaouleta (fu. 9). Ni mtume Yohana pekee yake ambaye hakuuawa, akiishi na kufikisha takribani miaka 90. (Soma mfululizo wetu wa wapanda farasi wa Ufunuo 6—DINI YA UONGO, VITA, NJAA na NDWELE.)
Hakuna mtu anayeweza kutilia shaka kwamba mambo haya sasa yanatokea kwa wingi sana kuliko huko nyuma. Kwa mfano, ni mara nyingi kiasi gani tunasikia juu ya matetemeko yenye kuleta uharibifu mkubwa? Mchambuzi mmoja maarufu wa vipindi vya runinga aliwahi kusema kuwa “kuna sababu fulani” kwamba matetemeko yanatokea zaidi duniani sasa. Wataalamu wa mitetemeko hutaarifu matetemeko tofauti 12,000 kila siku.
Mpya, milipuko ya magonjwa hatari ya zamani—mengi kati ya hayo sasa yamejenga usugu dhidi ya dawa­—yanaripotiwa mara nyingi zaidi. Magonjwa haya ni pamoja na janga la UKIMWI, Kipindupindu, Homa ya Matumbo, Homa ya Dengu, bacteria wala nyama, Ebola na virusi vya Naili Magharibi, Malaria, Ugonjwa wa Miguu na Midomo, Ugonjwa wa Kichaa cha Ng’ombe, kurudi kwa Kifua Kikuu kikali zaidi kisichosikia dawa na mlipuko wa magonjwa ya ZINAA (magonjwa yaambukizwayo kwa ngono). Haya ni sehemu ndogo ya picha kubwa ya magonjwa mapya ya kutisha ambayo bado yanaibuka—na ya zamani yakirudi na kisasi!
Zaidi ya watu 200,000 sasa, hufa kila siku kwa njaa—idadi hii ikiendelea kuongezeka! Vita, na kile ambacho mwandishi wa injili Luka alikiita “fitina” [vurugu au ghasia] (21:9), sasa hujaza vichwa vya magazeti—zikileta mateso zaidi na vifo. Magonjwa na vifo vitokanavyo na kukosa chakula ni madhara yatokanayo na watu kuhama makazi yao na mkanganyiko ambao daima hufuatia mwanzo wa vita.
Katika miaka ya hivi karibuni, wanasayansi wameonya dhidi ya hatari ya kuongezeka kwa joto duniani. Ni wachache ambao bado wanatilia shaka kwamba hali mbaya ya hewa tayari imeikumba dunia. Tufani ni kali zaidi na zinatokea mara kwa mara. Mafuriko yasiyo ya kawaida na uharibifu wa ardhi unasababisha njaa na majanga ya magonjwa ambayo hayajawahi kusikiwa. Majanga ya hali ya hewa, matetemeko, vita na magonjwa yatokanayo na hayo na kukosa matumaini huzidisha kile ambacho tayari ni mlipuko wa mateso. Unabii pia ulitangulia kusema kuwa hata milipuko ya volkano itaongezeka—na hii inatokea!
Ulimwengu unahitaji Sheria za Mungu, ambazo kama zingetunzwa na mataifa yote, ingeleta amani kote, furaha, wingi wa chakula na mafanikio. Miji ingekuwa mizuri. Magonjwa, njaa na vita vingetoweka, na ndivyo ingekuwa kwa ubaguzi wa rangi, ujinga, umaskini na kila aina ya dini za uongo.
Bado, hakuna mwanadamu, wala serikali ama serikali zote za wanadamu kwa pamoja zinaweza kuleta mambo haya!
Ni ufalme wa Mungu pekee, ukiongozwa na Kristo na watakatifu ambao wamefuzu kuungana naye, wataleta mambo haya. Ni lazima ulimwengu ujifunze juu ya Sheria za Mungu. Isaya 2:2-4 na Mika 4:1-4 pia huongelea juu ya “siku za mwisho,” wakati mambo haya yatakapotokea. Sheria za Mungu na pendo la Mungu (Rum. 13:10) vimetabiriwa kuchukua nafasi ya hali ya watu kutotii sheria na chuki ambavyo sasa vinatawala miongoni mwa watu na mataifa duniani!
Kama hataingilia kati, Kristo alisema kwamba, “Na kama siku hizo zisingalifupizwaasingeokoka mtu yeyote [bakia hai]; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo” (Math. 24:22)!
Fikiri! Ni lini mwanadamu ambapo amekuwa na uwezo wa kuangamiza maisha ya wote wenye mwili? Ni mpaka pale kulipovumbuliwa silaha za kisasa za nyukilia, kemikali, kibaiolojia na sasa “kiradiolojia” hili lawezekana. Tunaishi zama ambayo haya yote yapo—na idadi ya silaha za nyukilia zilizopo peke yake sasa zaweza kuangamiza wanadamu wote mara nyingi sana! Kama kiongozi mmoja alivyosema, “Mara moja ingetosha kabisa.”
Baadhi hupendekeza kwamba silaha hizi ni mbaya mno kuwahi kutumika—kwamba zipo tu kama “kipingamizi” dhidi ya matumizi yake”.
Usidanganyike! Zitatumika. Unabii mwingi unaweka jambo hili wazi. (Kumbuka, mara silaha hizi zilipopatikana, Marekani iliona vyema kuzitumia, Rais Truman aliamuru zitumike katika mwezi wa August 1945­—bila kusita! Lakini, mabomu mawili yaliyoanguka nchini Japani yalikuwa kama “njiti ya kiberiti” ikilinganishwa na zile zilizoko leo.)
Si kwa bahati tu kwamba injili ilihubiriwa ulimwenguni kote muda ule ule silaha za maangamizi zilipopatikana—zikithibitisha katika muda mwafaka usahihi wa onyo la Kristo juu ya hatari inayotishia uwepo wa mwanadamu!

Dhiki Kuu Inayokuja

Ikielezea wakati ambapo injili ya ufalme wa Mungu haitahubiriwa tena (24:14), Mathayo 24:21 inajumuisha onyo juu ya Dhiki Kuu inayokuja. Hii ilitamkwa kabla ya kauli ya Kristo kwamba siku za mwisho zitafupizwa. Angalia: “Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.”
Hii inaonyesha wakati mgumu kabisa kwa kila kiumbe chenye uhai duniani!
Kijitabu hiki kwa urahisi kabisa kingeweza kuwa kirefu kama hata kisehemu cha aya nyingi zinazoelezea hali za kutisha zinazokuja duniani zingenukuliwa hapa. Karibu kila nabii katika Agano la Kale aliongelea juu ya wakati huu wa machafuko duniani, yatakayotokea hivi karibuni. Muda unakwisha!

Unabii Mrefu wa Danieli

Unabii mrefu kuliko mwingine ndani ya Biblia unapatikana katika Danieli 11. Sura ya 10 huutambulisha na sura ya 12 huukamilisha. Mara nyingi (mara sita katika sura ya 12 pekee) neno “mwisho” linapatikana. Kwa mara ya kwanza “wakati wa mwisho” huonekana katika Danieli 11:40.
Lakini nabii Danieli hakuruhusiwa kuelewa unabii aliouandika. Alipomwuliza Mungu (12:8) maana yake, Mungu alimwambia kuwa ulikuwa “umefungwa mpaka wakati wa mwisho” (fu. 9). Ulipaswa kufunguliwamara wakati huo ulipowadia—na hii imetokea. Fungu la 10 linafundisha, “walio na hekima wataelewa” lakini kwamba “hataelewa mtu mbaya awaye yote.” Hii ina maana kwamba baadhi—wachache sana kwa kulinganisha—wataelewa, ili hali wengi hawatauelewa unabii wa Daniel!
Danieli 12:4 hutoa viashiria viwili muhimu vinavyowezesha kujua wakati wa mwisho utakapokuwa umefika. Angalia: “Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.”
Tumekwisha kujadili mlipuko wa ajabu wa maarifa ulioletwa na kupatikana kwa kompyuta katika mamilioni ya familia. Watu wengi sasa wanaweza kuyafikia maarifa ya aina nyingi—mara moja! Kile ambacho kinachoweza kueleweka haraka kwa mtu yeyote anayetafuta habari kinatisha! Kwa hakika tumefikia wakati ambapo “maarifa yataongezeka”—sambamba na upatikanaji wake kwa urahisi!
Daniel pia aliandika, wengi wataenda mbio huko na huko.” Ilianza na kupatikana kwa usafiri wa reli katikati ya karne ya kumi-na-tisa—kisha meli kubwa zikiendeshwa haraka na injini zenye nguvu kukatisha bahari—ikifuatiwa na magari—na hatimaye, ndege zilizoifanya sayari yetu kufikika karibu kila mahali. Kuwasili kwa ndege aina ya Konkodi zenye kasi ya ajabu kuliifanya bahari ya Atlantiki iwe kama ziwa kubwa. Ni wazi sasa kuwa, sayari inaendelea kuwa ndogo kila siku kwa sababu ya uwezekano wa watu “kukimbia huko na huko” karibu kila mahali na wakati wowote!

Falme Nne Zilizotabiriwa

Kitabu cha Danieli pia huongelea unabii mwingine mkuu katika Biblia. Sura ya pili ina unabii unaochukua zaidi ya miaka 2,500, ukikamilika na Kurudi kwa Kristo Mara ya Pili. Unabii huu unaonyesha picha ya jitu kubwa lililoundwa kwa madini ya aina nne (dhahabu, fedha, shaba, na chuma kilichochanganyikana na udongo wa mfinyanzi), linalowakilisha falme kuu nne zenye kutawala dunia yote zilizoanza kwenye wakati wa Danieli.
Ufalme wa kwanza, uliokuwa kichwa cha dhahabu, uliwakilisha ufalme wa Kibabeli wa Nebukadneza, au Himaya ya Wakaldayo (625-538 KK). Kifua na mikono ya fedha viliwakilisha ufalme wa pili au Himaya ya Waajemi (558-330 KK), uliofuatia, wakati tumbo na mapaja ya shaba viliwakilisha ufalme wa tatu wa Wagiriki (333-31 KK) au Himaya ya Ugiriki-na-Makedonia (iliyoongozwa na Iskanda Mkuu). Mwisho, ufalme wa nne, uliosimamiwa na miguu ya chuma, na nyayo na vidole vya chuma kilichochanganyika na udongo wa mfinyanzi, uliwakilisha Himaya ya Kirumi. Himaya hii ya mwisho iliyo kuu kuliko zote iliishinda na kuchukua mahali pa Himaya ya Ugiriki-na-Makedonia. Vidole kumi vya miguu vinawakilisha mataifa au falme kumi tofauti katika Ulaya Mashariki na Ulaya Magharibi. (Himaya ya Kirumi ilikuwa na makao makuu sehemu mbili—Katika mji wa Roma na Konstantinopo.) Ni huu muunganiko wa kidini na kisiasa ki-matifa ambao utaunda vidole kumi—chini ya kiongozi mkuu wa mwisho, akisaidiwa na mwingine wa pili mwenye kutenda miujiza duniani. Mfumo huu wa Dola yenye nguvu unajiunda katika jukwaa la ulimwengu sasa.
Danieli 2:34 na 44 huthibitisha kwamba vidole hivi vya miguu vinakuwepo wakati wa Kuja kwa Kristo. Mafungu haya yanaelezea jiwe kubwa linalokuja kutoka mbinguni na kuvunja vunja vile vidole kumi vya miguu—kuchukua mahali pake—na kusimamisha ufalme wa Mungu duniani. Lugha hii ya picha inaonyesha Kurudi kwa Kristo na kusimika serikali ya Mungu yenye nguvu itawalayo ulimwengu mzima—ikifutilia mbali serikali zote zilizobuniwa na wanadamu!
Kristo alipoongelea juu ya “mwisho wa ulimwengu” (Math. 24:3), alikuwa akirejelea mwisho wa USTAARABU WA MWANADAMU—alikuwa hatoi unabii wa sayari “kusambaratika.”
Ni kwa kulinganisha Ufunuo 13, 17 na Danieli 7, pamoja na Danieli 2 tu, ndipo unaweza kuelewa fika upana na uzito wa unabii huu. Maandiko mengi hurejelea falme hizi nne, lakini sura hizi huzielezea vizuri zaidi.
Kwa ufupi, Himaya ya Kirumi (ambayo ilianza mwaka wa 31 KK) ilianguka mwaka wa 476 BK—ikiwa imeshindwa na falme tatu (pembe) kutoka Ulaya Kaskazini zilizojulikana kama Vandos, Heruli naOstrogoths. Danieli 7:8 inaonyesha kwamba pembe hizi tatu “zikang'olewa kabisa.” Hii inamaanisha kuwa zilipotea kabisa katika historia. (Wavandos walikuwa wabaya na waharabu kiasi kwamba neno la kiingereza kipya “vandalize” [uharabu wa kishenzi] lilitokana na jina lao.) Hata hivyo, pembe saba zaidi (fungu la 7 husema zilikuwepo pembe kumi) zilitabiriwa kuitawala himaya hii.
Kuanzia mwaka wa 554 BK, Himaya ya Kirumi ilijulikana kama Himaya Takatifu ya Kirumi. Wanahistoria wanakiri kwamba Kitendo cha Papa kumtawaza Justinian kuwa mtawala kiliashiria mabadiliko haya. Matukio katika Ulaya, yaliyohusiana na Himaya Takatifu ya Kirumi, yaliibuka na kuanguka kwa karne nyingi. Kitambo baada ya kitambo, watawala wapya walitokea—Shalomeni (kichwa cha Kifaransa mwaka 800 BK)—Otto Mkuu (kichwa cha Kijerumani aliyetawazwa mwaka 962 BK)—akifuatiwa na Utawala wa Habsburg wa Charles V (kichwa cha Austria aliyetawazwa mwaka 1520 BK)—ambao, hatimaye ulifuatiwa na utawala wa Napoleoni (kichwa cha Kifaransa aliyetawazwa mwaka 1805)—pamoja na kichwa cha sita kikiwa ni Garibaldi kilichounganisha Italia kutoka 1870-1945 BK! Ufufuko huu wa sita wa Himaya Takatifu ya Kirumi uliishia kwenye kumshinda Adolf Hitler na dikteta wa kiitaliano Benito Mussolini. Mussolini, baada ya kutia saini makubaliano ya siri (Konkodati) na Vatikani mwaka 1929, aliiunganisha Ethiopia, Eritrea na nchi ya kiitalia ya Somalia na kuzirudisha kwenye mamlaka ya Italia mwaka 1935. Aliutangaza muungano wake huu kama Himaya ya Kirumi iliyosimamishwa upya!
Himaya hii imetabiriwa kutokea tena mara moja zaidi—ni kufufuka mara moja tu kwa Himaya Takatifu ya Kirumi kulikosalia!
Ni ile pembe ya kumi tu ya Danieli 7:7 (sawa na vile vidole kumi vya miguu vya Danieli 2) ndiyo ambayo haijatokea. Huyu ndiye atakayekuwa mnyama mkubwa wa mwisho wa Ufunuo 17 atakayetokea kwa ulimwengu usiokuwa na habari kwa nguvu na kasi ya ajabu (Ufu. 17:12). Kufuatia kuanguka kwa Pazia la Chuma na kuungana kwa Ujerumani mwaka 1989, kufufuka kwa mara ya mwisho kama Muungano wa Nchi Huru za Ulaya, kutakakohusisha nchi na falme kutoka Ulaya Mashariki na Magharibi, kuko karibu kutokea. Lakini tumekwisha kusoma namna ambavyo Kristo atauponda ponda muungano huu wa falme za kibinadamu wakati wa Kuja Kwake.

Onyo la Petro

Katika 2 Petro 3:3-4, Petro aliandika, “Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao TAMAA zao wenyewe, na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake?”
Ulimwengu wa leo umejaa watu wenye kudhihaki. Hawaamini kwamba Mungu ataingilia kati—au hata kwamba jambo hili ni la lazima! Wengi wanaamini kuwa ubinadamu unao uwezo katika dakika za mwisho “kunyakua ushidi kutoka makucha ya simba [kushindwa],” na utaweza kujiokoa na kutatua matatizo yake! Wengi wanaamini kuwa hatimaye mambo yote yatakaa sawa—kwa namna fulani!” Katika muda mfupi, mwanadamu hukosea—lakini katika muda mrefu, yuko SAHIHI!
Watu hudhihaki lile wazo kwamba Kristo anakuja—na huchagua kuishi mtindo wa maisha machafu ya dhambi, “wakifuata tamaa zao wenyewe”—lakini dhihaka zao hazitabadilisha ukweli wa unabii ulio katika kijitabu hiki! Wanadamu lazima wajifunze masomo machungu—kwamba wameshindwa kuleta yale ambayo kila mmoja anayatamani duniani. Amani, furaha, mafanikio na vyakula tele hubakia kama ndoto licha ya juhudi zisizokoma za mwanadamu kuyatafuta.
Majeshi “yakijaribu kuifanya dunia iwe salama kwa ajili ya demokrasia,” misaada ya kibinadamu, wamishenari, “jumuiya za washauri mabingwa,” vifaa vipya vya kisayansi vya kumpunguzia mwanadamu kazi, kompyuta, simu za mkononi, mifumo bora ya elimu, harambee kuchangia juhudi za kutokomeza magonjwa, n.k., zote zitashindwa. Hii ni kwa sababu ubinadamu hauko tayari kunyenyekea na kumtafuta Mungu ambaye pekee yake analo suluhisho kwa matatizo ya mwanadamu!
Ni pale karibu kabisa na kuchelewa, Kristo ataingilia kati kwa nguvu nyingi na utukufu kumwokoa mwanadamu kutoka kwa yeye mwenyewe!

Vipi Kuhusu Wewe?

Vipi kuhusu wewe? Utafanya nini kujiandaa na yale yaliyo mbele yako? Hakuna mtu wa kudai hana nguvu za kujiandaa mwenyewe kwa ajili ya kile kinachokuja. Danieli 12:1-2 ina kauli hii: “Wakati huo…kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu [wa Mungu] wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele.”
Fungu hili linaelezea ufufuo wa wafu—wa watakatifu wa kweli wa Mungu—watakaotawala pamoja na Kristo (Dan. 7:18, 22, 27)! Paulo aliandika, “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko…nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi [watakatifu walio hai katika Kanisa la Mungu] tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele” (1 Thes. 4:16-17).
Maandiko ya Agano Jipya yanaonyesha kwamba Kuja kwa Kristo Mara ya Pili kutakuwa kwa kushitukiza bila kutegemewa. Mara kwa mara Kristo amesemwa akija “kama mwivi usiku.” Soma kwa makini Mathayo 24:43-44, 1 Wathesalonike 5:2, 4, 2 Petro 3:10 na Ufunuo 3:3, 16:15. Katika maelezo sambamba ya Luka kuhusu Unabii wa Mlima wa Mizeituni aliandika pale Kristo alipokuwa akielezea Kurudi Kwake kwa ulimwengu usiokuwa na habari: “Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu…kwa kuwa kama mtego ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima. Basi, KESHENI ninyi KILA WAKATI, MKIOMBA, ili mpate kuhesabiwa kustahili KUOKOKA na haya yote yatakayotokea, na KUSIMAMA MBELE ZA MWANA WA ADAMU” (Luka 21:31, 35-36).
Fungu hili laweza kuwa mstakabali wako!
Wewe ndiye “nahodha wa meli yako mwenyewe” na “mwamuzi wa hatima yako mwenyewe”—ama utachagua kulikataa onyo la Mungu au kujisalimisha mwenyewe kwake na kumwomba akuandae kwa ajili ya utawala katika ufalme wake!
(Soma vijitabu vyetu vya bure Ni Nani au Nini Mnyama wa Ufunuo?Mashariki ya Kati Katika Unabii wa Biblia na Hatimaye Ufunuo Wafafanuliwa! kufahamu kwa undani zaidi matukio yaliyoelezewa katika kijitabu hiki. Vile vile soma Ulimwengu wa Kustaajabisha wa Kesho – Taswira ya Ndani! ili kuona picha kubwa yenye kutia hamasa juu ya namna ambavyo Mungu atatatua kila tatizo kubwa la Mwanadamu, kwa wakati wote.)

Watakatifu Watatawala Pamoja na Kristo—Duniani

Maelezo yafuatayo yanatoka kwenye hitimisho la kijitabu cha Herbert W. Armstrong JeTuko Kwenye Siku za Mwisho? Ni muhtasari mzuri wa nini kinachokuja mwisho wa miaka 6,000 aliyotengewa mwanadamu:
“Na tunaenda wapi baada ya kutoka hapa? Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki (Zak. 14:4).
“Tunasoma katika Ufunuo 20:1-2 kwamba muda huo wa Kurudi kwa Kristo, Shetani ataondolewa kutoka kiti cha enzi cha utawala wa dunia. Kisha Yesu Kristo ataketi katika kiti hicho cha enzi na kutawala juu ya dunia nzima. Katika Ufunuo 3:21, Yesu aliwaambia wale walio kwenye kanisa lake la kweli, kwamba kama tutamshinda Shetani na maovu ya dunia hii, atatupatia kuketi pamoja naye kwenye kiti hicho cha enzi.
“Vile vile Yesu alisema katika Ufunuo 2:26-27 kwamba kama sisi, watu wake mwenyewe, tutashinda tutapewa mamlaka juu ya mataifa, na tutawatawala, chini ya Kristo. Katika Ufunuo 5:10, anasema kwamba sisi ambao ni waumini wa kweli katika kanisa lake mwenyewe tutakuwa makuhani na wafalme, na tutatawala duniani.”

Maoni 1 :

 
 
Blogger Templates