Kitu kambani: Winga wa Scotland, Ikechi Anya akipiga mpira uliompita kipa wa Ujerumani Manuel Neuer na kuisawazisha bao.
MABAO mawili ya Thomas Muller yalitosha kuwapa ushindi Ujerumani dhidi ya Scotland katika mechi ya kwanza ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2016 (Euro 2016).
Muller alifunga bao la kwanza katika dakika ya 18 ya mchezo, lakini Ikechi Anya akaisawazishia Scotland katika dakika ya 66.
Baada ya matokeo kuwa 1-1, Ujerumani ambao ni mabingwa wa kombe la dunia chini ya kocha Joachim Low walifanya mashambulizi kadhaa langoni kwa Wascotish na katika dakika ya 70, Muller aliandika bao la pili na la ushindi.
Bahati mbaya kwa Scoltland ilitokea ambapo walijikuta katika dakika za majeruhi wakicheza pungufu baada ya Charlie Mulgrew kuoneshwa kadi nyekundu.
Hisia kali: Anya alionekana kutoamini baada ya kuifungia Scotland bao la kuaswazisha dhidi ya mabingwa wa dunia Ujerumani
Ukiujua mpira unaweka kiulaini tu: Thomas Muller akifunga bao la pili wakati zikisalia dakika 20 ngoma kumalizika
Watu kimyaaa!: Muller akishangilia baada ya kuiokoa Ujerumani kwa kuifungia bao la pili dakika nne tu baada ya Scotland kusawazisha
Kikosi cha Germany (4-3-3): Neuer 6, Rudy 7, Howedes 7, Boateng 7, Durm 7, Kroos 7, Kramer 7, Gotze 7, Reus 7 (Ginter, 90), Schurrle 6, (Podolski, 84), Muller 8.
Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Zieler, Grosskreutz, Sam, Rudiger, Gomez, Weidenfeller.
Mfungaji wa mabao: Muller, 18, 70.
Kadi ya njano: Durm, Muller.
Kocha: Joachim Low, 7.
Kikosi cha Scotland (4-5-1): Marshall 7 Hutton 6, R Martin 6, Whittaker 6, Hanley 6, Mulgrew 6, Morrison 6, D Fletcher 5 (McArthur, 57), Bannan 5 (S Fletcher, 57) Anya 8, Naismith 7.
Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: A McGregor, Greer, Maloney, Bryson, McDonald, Burke, Reynolds, Forsyth, C Martin, Gordon.
Kadi ya njano: Hanley.
Kadi nyekundu: Mulgrew.
Kocha: Gordon Strachan, 6.
Mfungaji wa goli: Anya, 66.
Mwamuzi: Svein Oddvar Moen (Norway), 6.
Mchezaji bora wa mechi: Thomas Muller
Watazamaji: 65,000
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni