Social Icons

Jumatano, 10 Septemba 2014

BUNGE MAALUM LA KATIBA LAENDELEA NA MJADALA WA RASIMU YA KATIBA.

pix 7
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akitoa maelezo muhimu wakati wa mjadala wa Bunge hilo leo 10 Septemba, 2014 Bungeni mjini Dodoma.
PIX 15,
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiingia ndani ya Bunge hilo leo 10 Septemba, 2014 kwa ajili ya kuendelea na mjadala wa Rasimu ya Katiba.
………………………………………………………

 
BUNGE Maalum la Katiba leo tarehe 10 Septemba, 2014 limeendelea na kazi yake ya kusoma na kujadili taarifa za Kamati mbalimbali Bungeni mjini Dodoma.
 
Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa katika Bunge hilo ni pamoja masuala ya migogoro ya ardhi inayowahusisha wafugaji na wakulima, mambo ya Uraia pacha, haki ya afya, haki ya kuishi ikiwemo sheria ya kunyonga, haki za binadamu, haki ya Mtuhumiwa na Mfungwa, haki za wafanyakazi na ajira pamoja umri katika ajira pamoja haki za vijana.
 
Akizungumza wakati wa mjadala huo, Mjumbe wa Kamati namba Sita, Mhe. Zaina Madabida amesema kuwa ni vema kuwepo kwa kipengele kinachotambua mila na desturi za makundi ya wafugaji na wakulima ili kuondoa migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara hapa nchini.
 
Kuhusu masuala ya Uraia, Mhe. Madabida ameeleza kuwa si vema kumtambua mtoto mwenye miaka Saba kama raia Mtanzania aliyekanyaga katika ardhi ya Tanzania na badala yake ni vema mtoto mchanga ndiyo atambulike kama raia halisi wa Tanzania kikatiba kama Mtanzania, hivyo yeye na Kamati yake wamekubaliana kumtambua mtoto mchanga kama Mtanzania halisi ambaye atakuwa amekanyaga katika ardhi ya hiyo.
 
“Mtoto ambaye ni raia halisi wa Tanzania atakayekutwa katika ardhi ya Tanzania itambulike kuwa ni yule mtoto mchanga na sio yule mwenye umri wa miaka Saba”, alisema Mhe. Madabida.
 
Aidha, Mhe. Madabida amegusia suala la Sheria ya Haki ya kuishi pamoja na Sheria ya kunyonga akisema kuwa Sheria hiyo ya kunyonga ni vema iendelee kuwepo katika Katiba kwani kuna watu ambao wao wanaua wenzao.
 
“Adhabu ya kifo iendelee kuwepo kama Katiba yetu ya sasa inavyosema kwani kuna watu wao wamekuwa wakiwaua wenzao”, alisema Mhe. Madabida.
 
Kwa upande mwingine, mjumbe toka kamati namba Tisa amezungumzia kuhusu suala la haki za binadamu akitaja Ibara ya 24 katika Sura ya Nne, nae amesema kuwa maoni ya wachache yamefafanua kuwa haki ya kuishi ianzie tangu pale mimba inapotungwa kwani sikuhizi watu wengi wamekuwa na utaalamu sana katika kutambua viumbe vilivyopo tumboni, hivyo watu hao wamekuwa wakikatiza uhai wa viumbe wasiokuwa na hatia.
 
Mjumbe ameongeza kuwa katika Ibara ya 39 inayohusu haki ya Mtuhumiwa na Mfungwa, yeye na kamati yake wameitaka Katiba izingatie mazingira rafiki kwa watuhumiwa wenye ulemavu na izingatie kuhusu suala la miundombinu kwa walemavu hao ili iwe rafiki kwani Magereza mengi nchini yalijengwa kipindi kirefu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates