Mlinda lango mweusi ambaye alibaguliwa kirangi katika mechi moja kubwa nchini Brazil amekataa msamaha kutoka kwa mmoja ya mashabiki waliohusika na kitendo hicho.
Shabiki huyo wa kilabu ya Gremio ,Patricia Moreira amepoteza kazi yake na kutishiwa maisha baada ya kuonekana katika camera akimwita mchezaji huyo wa kilabu ya santos ,Aranha,Tumbili.
Amesema kuwa alitaka kukutana na mchezaji huyo ili kumuomba msamaha binafsi,lakini Aranha amekataa ombi hilo akitaka mashabiki waliohusika na kitendo hicho kuadhibiwa vilivyo.
Bi,Moreira amesema kuwa alilazimika kutoa matamshi ya hayo ya ubaguzi wa rangi wakati timu yake ilipokuwa ikishindwa katika mechi ya kuwania taji.
Kilabu ya Gremio imepigwa marufuku katika mashindano hayo huku mashabiki ambao watajulikana walitoa matamshi hayo ya kibaguzi wakipigwa marufuku ya kuona mechi za soka kwa miaka miwili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni