Social Icons

Jumapili, 21 Desemba 2014

Mohammed Ali alazwa hospitalini

Aliyekuwa bingwa wa ndondi duniani Mohammed Ali na Mwanawe leila Ali.Bondia huyo mkongwe amelazwa hospitalini akiugua maambukizi ya mapafu.
Aliyekuwa bingwa wa ndondi ulimwenguni Mohammed Ali amelazwa hospitalini baada ya kuugua maambukizi ya mapafu.
Ali ambaye ana umri wa miaka 72 na ambaye ana ugua ugonjwa wa Parkinson anadaiwa kuwa katika hali imara .
Msemaji wake amesema kuwa ugonjwa huo uligunduliwa mapema.
Mohammed Ali wakati wake alipokuwa bingwa wa ndoni duniani.
Hatahivyo hakutoa maelezo zaidi na kutaka haki ya faragha ya familia ya bondia huyo mkwongwe kuheshimiwa.
Ali alipataikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka 1984,miaka mitatu baada ya kuustafu katika masumbwi.
Alionekana hadharani katika sherehe moja mnamo mwezi Septemba nyumbani kwake Louisville Marekani wakati wa kutoa tuzo za kibinaadamu za bondia huyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates