Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Taifa Mh Mboni Mhita Ambaye Pia ni Katibu Mkuu wa Pan African Union Ulio Chini ya Umoja wa Afrika AU Anayehusika Kushugulikia Ajira kwa Vijana, Fursa ,Elimu Afya na Mambo yanayuwahusu Vijana Akiwasikiliza Kwa Makini Viongozi wa Mtandao wa wafanyabiashara Ndogondogo Kutoka Mkoani Dar Es salaam Aliokutana nao Leo Kusikiliza Changamoto zinazowakabili Vijana hasa Wafanyabiashara Ndogondogo Maarufu Kama wamachinga walioipigwa Mabomu ya Mcahozi jana na Jeshi la polisi,Katika Kiako Hicho Viongozi wa wafanyabiashara Ndogondogo wameeleza Changamoto zinazowakabili kama Ukosefu wa Maeneo ya Kufanyia Biashara ,Kutokutambuliwa na Idara Yoyote ya serikali ,
Kutokusajiliwa .
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Taifa Mh Mboni Mhita Amezichukua changamoto hizo kwenda kujadiliana na wadau mbalimbali kuona namna ya Kuzitatua ili Wafanyabiashara hao waweze kufanya biashara kwa uhuru na haki bila kubugudhiwa na watendaji wachache wanaowatumia wafanyabiashara hao kwa maslai yao Binafsi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa wafanyabiashara Ndogondogo Kutoka Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Job Mwakatobe Akimweleza Mh Mhita Changamoto Kubwa Zinazowakabili wafanyabishara hao hali Iliyopelekea Sitofahamu Mpaka Kupigwa Mabomu ya Mcahozi jana
Viongozi wanaounda Mtandao wa Umoja wa wafanyabiashara Ndogongodo wakijadiliana Jambo katika Kiakoa hicho.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Taifa Mh Mboni Mhita Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Viongozi hao leo Maraekanavyo. baada ya kuwasiliza na Kuchukua changamoto zianzowakabili wafanyabiashara hao kwa lengo la kwenda kuzifanyia kazi haraka iwezekanavyo.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Taifa Mh Mboni Mhita Akiwa na Viongozi wa Mtandao wa wafanyabiashara Ndogondogo Mkoani Dar es Salaam wakiwa Eneo la machinga Complex Kujionea hali hali mara baada ya Viongozi hao kumweleza ya kumwa Eneo Hilo lilijengwa Maalum kwajili ya wamachinga lakini cha kushangaza Wamepangishwa wafanyabiashara Wakubwa na Maofisi
Mh Mboni Mhita Akizungumza na Wafanyabiashara Ndogondogo aliotembelea Eneao hilo na kukuta Sehemu Kubwa Ikiwa Haina watu
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Taifa Mh Mboni Mhita Akishuhudia Jengo Malum la Wafanyabiashara Ndogondogo la Machinga Complex likiwa Tupu wakati wafanyabiashara hao hawana Maeneo ya Kufanyiabishara ikielezwa Kwamba chanzo cha Jengo Hilo kuwa wazi ni Urasimu wa Namna ya Kupata eneo la Kufanyia Biashara
Maeneo ya wamachinga yakiwa katika Hali Mbaya Enewo la Ilala
Mh Mboni Mhita akishuhudia Mazingira Magumu ya Kufanyia Biashara.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Taifa Mh Mboni Mhita Akiagana na Viongozi wao wakipeana Mkakati wa namna ya Kutatua Changamoto zinazowakabili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni