Social Icons

Jumamosi, 5 Oktoba 2013

AJALI HIZI MPAKA LINI?

ANGALIA PICHA ZA AJALI MBAYA MLIMA KITONGA,KAMA UNAMOYO MWEPESI TAFADHALI SAMAHANI KWA PICHA HIZI.

Ajali mbaya nyingine imetokea usiku huu katika mlima kwa Kitonga wilaya ya Kilolo mkoani Iringa katika barabara kuu ya Dar es Salaam -Iringa jana .
 
Katika ajali hiyo watu wawili wamekufa papo hapo huku wa wawili wakijeruhiwa vibaya baada ya malori mawili kugongana uso kwa uso .
 
Ajali hiyo imetokea mida ya saa 12.50 jioni ya jana ikiwa ni dakika takribani 30 baada ya ajali ya basi la JM kupinduka eneo la Mazome wilaya ya Kilolo.
 
waliopoteza maisha katika ajali hiyo ambayo chanzo ni dereva wa lori la IT lililokuwa likisafirishwa kwenda nchi za kusini mwa Tanzania aliyekuwa akitaka kulipita gari la mbele mlimani na katika kona kali .
 
Hata hivyo dereva wa lori hilo IT aliyetambuliwa kwa jina la Gody amevunjika mguu wake ambao umetoka katika na dereva na utingo la fuso wame kufa papo hapo huku mwanamke aliyekuwa katika lori IT akisalimika .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates