Social Icons

Ijumaa, 4 Oktoba 2013

Ghasia Mombasa baada ya Sheikh kuuawa

Mmoja wa walionusurika baada ya Sheikh Ibrahim Ismael na wengine watatu kuuawa  Mombasa, Kenya, Oct. 3, 2013.
Mmoja wa walionusurika baada ya Sheikh Ibrahim Ismael na wengine watatu kuuawa Mombasa, Kenya
 
Waandamanaji katika mji wa Mombasa Kenya, wamechoma Kanisa moja na magurudumu ya magari , baada ya watu wenye silaha kumpiga risasi na kumuuwa kiongozi mmoja maarufu wa ki-Islam na washirika wake watatu.
Ghasia zilizuka leo Ijumaa, siku moja baada ya washambuliaji wasiofahamika kumfyatulia risasi Sheikh Ibrahim Amor na washirika wake wakati wakisafiri ndani ya gari moja karibu na Mombasa.

Mashahidi wanasema polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi hii leo na kuingia katika mapambano na vijana wa ki-islam katika kitongoji kimoja cha Mombasa.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya linasema mtu mmoja alifyatuliwa risasi na kuuwawa wakati wa ghasia hizo. Sheikh Amor alionekana kama mrithi wa Sheikh Aboud Rogo Mohammed, ambaye alihubiri kwenye msikiti huo huo mjini Mombasa , alishutumiwa kuwa kuwa na uhusiano na wanamgambo wa ki-Islam wa al-Shabab.

Ghasia zilizuka baada ya Rogo kuuwawa kwa kupigwa risasi mwaka 2012 katika barabara hiyo hiyo ambayo Amor aliuwawa hivi leo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates