Social Icons

Alhamisi, 3 Oktoba 2013

HALI YA UTULIVU YAREJEA JIJINI MBEYA , MKUTANO WA WAFANYA BIASHARA WASHINDWA KUFANYIKA.

Hali ya amani Imerejea jijini Mbeya muda huu baada ya Jeshi la Polisi Kudhibiti Vurugu hizo ambazo wafanya Biashara waliandamana kupinga Bei za Mashine za TRA, Utulivu huo umetokea baada ya Jeshi la Polisi Kutangaza kuwa kila mtu arejee kwao na kuwasihi wananchi wasifanye tena fujo hizo.

 Magari ya Jeshi la Polisi yakiwa yanazunguka kila upande kuhakikisha kuna usalama wa kutosha 

 Sasa safari za Daladala Mwanjelwa zinaendelea kama kawaida 
 Ulinzi mkali umeimarishwa pembezoni mwa Maduka ili kuepusha uharibifu wa vibaka ambao wanaweza vamia maeneo hayo
Huu ni moja ya mitaa ambayo imechangamka sana kwa Mfikemo lakini jana hali imekuwa kimya hakuna hata sehemu moja iliyo wazi kote kumefungwa .

 Hii ni Mitaa Mbalimbali ya Mwanjelwa ambapo Maduka yote yamefungwa hakuna aliye fungua siku nzima ya jana .

Gari la kumwaga maji ya kuwasha kutoka Jeshi la Polisi Likiwa limesimama tayari kwa lolote ambalo litatokea muda huu na mpaka baadae...

Mpaka sasa hivi tunapo toa ripoti hizi za moja kwa moja kutoka Jijini Mbeya  kutokana na vurugu kubwa iliyozuka kwa wafanya biashara kugomea mashine za TRA, Sasa wafanya biashara hao wamerejea makwao ingawa kulikuwa na vugu vugu la Vijana vibaka kuleta vurugu lakini nao Jeshi la polisi limeweza kuwadhibiti wote na hali sasa imekuwa tulivu... Ingawa kulikuwa na Minong'ono kutoka kwa watu mbalimbali wakiomba hali hii  iwe shwari na kusiwe na vurugu tena...



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates