Social Icons

Jumapili, 26 Oktoba 2014

POLISI YAKAMATA MABOMU MANNE YA KIVITA HUKO ZANZIBAR


Jeshi la polisi Zanzibar limefanikiwa kumkamata mtu mmoja akiwa na mabomu manne ya kivita ambayo yanasadikiwa ni miongoni mwa mabomu yanayotumika katika vitendo vya uhalifu yaliyotokea sehemu mbali mbali nchini.Kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar CP Hamdani Omar Makame amethibitisha kukamtwa kwa mtu huyo ambaye kwa Mujibu wa jeshi hilo mtu huyo amekiri kuwa anajishughulisha na  mtandao  wa kuagiza, kuingiza  na kuhifadhi  mabomu ya kivita ya kurushwa kwa mkono na mabomu hayo yalikuwa matano na polisi  wamesema huenda moja ya hilo likawa ndilo lilotumika Darajani huku kamishna akidai mtandao huo unausishwa na matukio kadhaa.


Hata hivyo kamishna Hamdani Maka amesema kukamtwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye hata hivyo amekataa kumtaja jina na mazingira ya ukamataji wake  amesema hausiani na imani ya kidini na polisi inamshughulikia mtu kisheria kutokana na kosa  lake  kwa mujibu wa sheria za nchi na siyo Imani za kidini.

Wakati polisi imekataa kutoa taarifa yeyote kuhusu mtuhumiwa huyo jeshi hilo limesema hakuna kosa lolote la kisheria endapo  mtu akipelekwa nje ya Zanzibar kwa kosa la ugaidi huku akisema bado polisi inaendelea na upelelezi  wa tukio hilo kama ni la Zanzibar  au la, ama ni mtandao wa ugaidi wa nchi nzima.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates