Social Icons

Alhamisi, 8 Januari 2015

KASEJA OUT YANGA.....................................

Uongozi wa Yanga rasmi umemtema kipa Juma Kaseja na kumtakia kila la kheri aendako.

Akizungumza mjini hapa, Mkurugenzi wa Habari wa Yanga, Jerry Muro amesema Kaseja amevunja mkataba kutokana na kutokwenda mazoezini kwa saa 48.

“Kaseja haidai Yanga na fedha zake aliishalipwa, tarehe zinaonyesha siku fedha hizo zilipolipwa.

“Pia katika mkataba hakukuwa na sehemu inaonyesha ni lazima Kaseja alipwe siku fulani lakini ilikuwa ni lazima alipwe ndani ya kipindi cha mkataba.

“Yeye aliamua kususa kuja kazini, jambo ambalo lilivunja mkataba wake na Yanga.
“Kwa kuwa hatudai, tumeona ni vema kumuachia aende andako na tunamtakia kila la kheri kama klabu ya Yanga,” alisema Muro.

Kaseja alijiunga na Yanga baada ya kuwa huru kutokana na Simba kumuacha.

Lakini aliamua kususia mazoezi baada ya Yanga kuchelewa kumlipa fedha zake za usajili zilizosalia.

Baada ya Kaseja kulipwa fedha alizokuwa akidai, aliandika barua kueleza amepokea fedha zake na alikuwa tayari kurudi kazini, lakini uongozi wa Yanga haukumjibu.

Kutokana na kuona hajibiwi, Kaseja alikwenda mazoezini lakini Kocha Marcio Maximo akamkataza kwa kusisitiza lazima awasiliane na uongozi wa Yanga.


Kaseja ni kati ya makipa wakongwe nchini ambao wamewahi kung’ara akiwa Simba na timu ya taifa, Taifa Stars.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates