Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Elliason akiwa pamoja na baadhi ya washiriki wa majadiliano hayo kushoto kwake ni Balozi Tuvako Manongi anaonekana pia Balozi wa Finland mwenye Tai nyekundu Bw. Kai Sauer
Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa akizungumza wakati wa majadiliano baina ya wajumbe wa Bodi ya Global Impact ambayo ni Taasisi ya Umoja wa Mataifa na Wawakilishi wa Balozi mbalimbali na kumshirikisha pia Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw, Jan Elliason.
Bw. Paul Polman CEO wa Unilever akizugumza wakati wa majadiliano hayo ambapo katika maelezo yake, alitambua juhudi za Serikali ya Tanzania za kujenga mazingira yanayoziwezesha sekta binafsi kukua na kuchangia maendeleo ya nchi.
Sehemu wa washiriki wa majadiliano hayo yaliyoambata na chakula cha mchana, majadiliano hayo yaliandaliwa kwa pamoja baina na Wakilishi za Kudumu za Tanzania, Finland na Bagladesh.
Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Bw. Songelael Shilla akiwa na washiriki wengine wa majadiliano hayo kuhusu nafasi ya sekta binafsi katika utekelezaji wa ajenda mpya za maendeleo endelevu na mchango wa serikali katika kuziwezesha sekta hizo kutekeleza majukumu hayo.
Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesisitiza kwamba, ili utekelezaji wa malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015 uwe wenye tija, Jumuiya ya Kimataifa inapashwa kulitafutia ufumbuzi tatizo la kuto kuaminiana baina ya serikali na wafanyabiashara.
Hayo yameelezwa mwishoni mwa wiki na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi wakati wa mkutano wa majadiliano wa Wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Umoja wa Mataifa ijulikanayo kama Global Compact waliokutana hapa Umoja wa Mataifa kwa Mkutano wao kwanza wa Bodi hiyo kwa mwaka huu.
Katika majadiliano hayo ambayo pia yalihudhuliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Elliason, Wajumbe wa Bodi na wawakilishi wengine zaidi ya 30 yaliandaliwa kwa pamoja baina ya Wakilishi za Kudumu za Tanzania, Finland na Bangladesh.
Balozi Manongi amesema kuna tatizo kubwa la kutoaminiana baina ya serikali na wafanyabiashara jambo analosema kama halitashughulikiwa linaweza kuathiri utekelezaji wa SDGs, utekelezaji ambao unahitaji sana ushirikiano na uhusiano kati ya sekta binafsi, serikali na wadau wengine.
Wakati wa majadiliano hayo wajumbe walibadilishana mawazo kuhusu wajibu na nafasi ya sekta binafsi katika utekelezaji wa ajenda mpya za maendeleo baada ya 2015. Aidha walijadiliana kuhusu nafasi ya serikali katika kutoa motisha kwa sekta binafsi ili kwayo ziweze kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa ajenda hizo za maendeleo.
Amesema msingi wa kiini cha mafanikio ya ushirikiano kati ya serikali na wafanyabiashara katika utekelezaji wa ajenda za maendeleo endelevu lipo suala la namna gani bora ya kushughulikia suala la kuaminiana miongoni mwa wadau.
Na kuongeza kuwa litakuwa jambo la muhimu sana kushughulikia sula hilo la upungufu wa kuaminiana miongoni mwa wadau na kwamba Taasisi hiyo ya Global Impact inayofursa nzuri na mchango wa mkubwa wa kutoa katika kujenga kuaminiana na kujiamini.
Akizungumzia juhudi za serikali katika utekelezaji wa sera ya ushirikiano na uhusiano kati ya serikali na sekta binafsi (PPP) na hasa kuelekea utekelezaji wa ajenda mpya za maendeleo, Balozi amewaeleza washiriki hao kuwa Tanzania siyo tu inatambua na kuthamini ushirikiano huo bali pia imjitahidia sana katika uboreshaji wa mazingira yanayoziwezesha sekta binafsi kutekeleza majukumu yake licha ya kukiri kwamba bado kuna mapungufu ya hapa na pale.
Akasema Tanzania inatambua kwamba serikali na wafanyabiashara wanatakiwa kufanya kazi kwa pamoja ili kujenga mifumo, sera na taratibu shirikishi zitakazotoa motisha kwa watendaji wa sekta binafasi kutoa mchago katika ukuaji wa uchumi endelevuvu na ujenzi wa viwanda ili kutoa ajira.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni