Moja ya timu za Majeshi – JKT Ruvu
Katibu mkuu wa Shirikisho la soka nchini, TFF, Celestene Mwesiga amesema kuwa kuanzia msimu ujao katika ligi kuu ya Tanzania hakuna mmliki mmoja ambaye ataruusiwa kumiliki timu zaidi ya moja kama ambavyo Shirikisho la soka Afrika, CAF na lile la ladunia FIFA walivyoagiza. Kwa maana hiyo timu kama JKT Ruvu, JKT Mgambo, Ruvu Shooting ambazo zote zipo chini ya umiliki wa jeshi la kujenga Taifa, zitapigwa mnada.
Sasa mmliki wa timu hizo atatakiwa kuchagua ni timu gani ambayo ataaiuza au kutengeneza kampuni mpya ya umiliki, na hazitaruhusiwa kucheza ligi kuu endapo zitaendelea kuwa chini ya umiliki mmoja kuanzia msimu ujao.
" Labda kwa faida ya Watanzania ili kueleweka vyema, hili si agizo ambalo limelenga timu za majeshi au timu za Polisi, ila ni zoezi la kutoa leseni kwa vilabu, halijalenga klabu. Mojawapo wa msingi wa kutoa leseni kwa klabu ni pamoja na kuepuka mtu mmoja kumiliki vilabu zaidi ya kimoja. Siwezi kisema kama ni leo hilo suala litafanyika lakini, lakini kila mshiriki, kila mdau ajue kabisa huko ndiko tunakoelekea. Kuanzia msimu ujao vilabu vyote vitakavyoshiriki ligi vitatakiwa kuwa na leseni. Huu ni utaratibu/maagizo ya CAF na FIFA ambao hawataki umiliki mmoja kwa vilabu zaidi ya kimoja kwenye ligi moja."
Katika kuonesha kuwa jambo hilo si la masihara TFF tayari imetoa taarifa kwa vilabu vyote, sasa ni wakati wa wamiliki ambao wanafahamu wanamiliki idadi ya timu zaidi ya moja kufanya utekelezaji wa utafutaji wa leseni hiyo ya ligi kuu.
" Hili linawahusu wamiliki wa bilabu vyetu au kokote pale Afrika kama kuna mmiliki mmoja ambaye anajijua ana vilabu ni lazima atafute namna ambayo umiliki huo utatenganishwa na kutokuwa chini ya mtu mmoja. Litafanyilaje, uamuzi wa kwanza ni wamiliki wenyewe kuamua ataendelea kuwa na timu ipi na ipi anaiuza au timu gani wataziunganisha"
Kuanzia msimu ujao timu za Manispaa ( mfano Mbeya City) hatakuwa mbili hivyo kutoa uwezekano wa timu kama Kuregenzi ya Mafinga kutocheza ligi kuu endapo itapanda na kuendelea kuwa chini ya Manispaa. Jeshi la Polisi pia litatakiwa kufanya uchaguzi wa timu ya kuendelea kumiliki kati ya rundo la timu walizonazo. Polisi Morogoro ipo katika ligi kuu msimu huu, wakati ligi daraja la kwanza lina timu kama Polisi Tabora, Polisi Mara, Polisi Dar es Salaam, Polisi Dodoma.
" Hilo linaanza msimu ujao. Hatuaziandikia barua timu Fulani tu, tumefanya hivyo kwa vilabu vyote. Idadi ya timu haitapungua katika ligi kuu, ila utafanyika utaratibu wa kutosha. Kwa mfano timu ambayo itabadilisha umiliki itaendelea kubaki katika ligi. Kama bahati mbaya itatokea bahati mbaya, timu ikafa, itaangaliwa namna ya kufanyika utaratibu mwingine. Tunaamini kuwa kutoa kwetu taarifa mapema kutafanya kusiwepo na timu yoyote itakayokufa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni