Mchuchumio’ ama viatu vyenye visigino virefu, ni mojawapo ya vitu vinavyopendwa na baadhi ya wanawake mbalimbali, sio Tanzania pekee bali dunia nzima.
Wataalamu wanaeleza kuwa viatu hivi huharibu pingili za uti wa mgongo na huvunjavunja mifupa ya visigino. Wanawake wenye maumbo ya kati, ambao si wanene wala wembamba wamekuwa wakipendelea viatu virefu. Kwa kiasi kikubwa wasichana wafupi, wamekuwa wakipendelea kuvaa viatu virefu ili angalau na wao waonekane warefu.
Ifaamike kuwa unapovaa viatu hivi uzito wa mwili uamia mbele ya mwili na kufanya nyonga isogee mbele na kumfanya mtu awe na kiuno kizuri na mgongo unaovutia hivyo kutegemea viatu hivi kwa muda uharibu umbo pale anapovaa viatu vya kawaida sambamba na Misuli ya visigino kukakamaa na kumfanya mtu aonekane na mguu mzuri ufunga vidole vya miguu na kusababisha maumivu makali chini ya mgongo na ulemavu wa vidole. Pia uweza kusababisha ugonjwa wa arthritisi kadiri umri unavyoongezeka na matatizo ya uzazi katika nyonga kutokana na kuelemewa na uzito asa kwenye jointi za magoti na nyonga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni