Social Icons

Alhamisi, 13 Novemba 2014

Ripoti ya FIFA kuhusu Qatar ina dosari

Wakili Machel Garcia
Ripoti ya shirikisho la soka duniani, kuhusu tuhuma za rushwa katika matifa kuwania nafasi ya kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 na 2011 imesemakana kuwa na dosari tele.
Mwenye kuhoji ripoti hiyo sio mwingine bali ni mtu aliyefanya uchunguzi huo wa miaka miwili kuhusu madai ya rushwa wakili Michael Garcia.
Katika kile ambacho hakikutarajiwa ni wakili Michael Garcia aliyefanya uchunguzi huo na ambaye anasema ripoti ya FIFA ambayo imeiondolea Qatar lawama zozote za rushwa ina makosa ,mengi na kwamba taarifa ambayo alitoa imevurugwa.
Ripoti ya FIFA yenye kurasa 42 iliiondolea lawama Urusi na Qatar ambazo zitakuwa wenyeji wa kombe la dunia mwaka 2018 na 2022.
Lakini ilituhumu shirikisho la soka la Uingereza kwa kwenda kinyume na utaratibu wa kutaka nafasi ya kuandaa michuano ya 2018 nma kuiharibia FIFA sifa.
Mkuu wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter
Katika ripoti yake shirikisho la soka duniani FIFA limeilaumu shirikisho la soka la Uingereza kwa kuvunja sheria za kutolewa kwa kibali cha kuandaa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2018.
Lakini shirikisho hilo liliiondolea Qatar lawama za rushwa wakati wa kupigania nafasi ya kuandaa kombe la dunia mwaka 2022.
Kwa mujibu wa ripoti ya shirikisho hilo, shirikisho la soka la Uingereza lilikwenda kinyume na utaratibu katika juhudi zake kutaka kupata nafasi ya kuandaa michuano ya kombe la duniani mwaka 2018.
Lilifanya hivyo ili kupata kura ya mmoja wa wadau mashuhuri.
Kwa upande wake Qatar ilikabiliwa na tuhuma nyingi tu, lakini taifa hilo sasa liko huru kuandaa michuano hiyo.
Kwa sasa ripoti iliyotolewa na FIFA inamaliza mgogoro kuhusu ikiwa kura nyingine itapigwa kuteua waandaji wa mashindano hayo katika miaka hiyo.
FIFA imeelezea kuwa mambo sasa yako shwari kufuatia uamuzi huo.
Maafisa wa Qatar wakisherehekea ushindi wa kuandaa kombe la dunia mwaka 2022
Qatar ilituzwa kuandaa kombe la duna mwaka 2022 mnamo 2010 na kuyapiku mataifa ya Australia, Marekani,Korea Kusini na Japani.
Uamuzi ulishangaza wengi na mwishowe kupelekea madai kadhaa ya rushwa, sio tu kuhusu mchakato wa zabuni za 2022 bali pia 2018.
Urusi ilishinda zabuni ya kuandaa mashindano ya mwaka 2018 na kuishinda Uingereza ambayo ilipata kura mbili pekee.
Qatar daima imekataa madai ya kufanya kosa, lakini uchunguzi ulianzishwa ukiongozwa na mchunguzi huru wa nidhamu Michael Garcia.
Mwanasheria huyo, raia wa Amerika pia alipewa kazi ya kuchunguza michakato ya zabuni ya kombe la dunia ya 2018 na 2022.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates