Social Icons

Jumanne, 20 Mei 2014

CHOKORAA KUPANDA ULINGONI MAY 24


Mwanamuziki na kiongozi wa bendi ya Mapacha watatu Kahalid chokoraa anategemea kupanda ulingoni jumamosi ya tarehe 24 katika ukumbi wa friends corner kuzipiga na bondia chipukizi mwenye uchu wa ushindi muda wote awpo ulingoni Abdul manyenza. Chokoraa alisema muda mrefu amekuwa akifanya mazoezi ya kujenga mwili na ya ngumi kwa muda mrefu na amekuwa akipigana na mabondia tofautitofauti mazoezini na kuona uwezo wao ni wa kawaida, 
hivyo anataka kuwaonesha kama ana kipaji kingine zaidi ya kuimbia, kwa sasa amekuwa akijifua katika gym ya bigright boxing ya mwananyamala chini ya mwalimu wake bondia mkongwe omar athuman ‘van dame’ kwa lengo la kumsambaratisha mpinzani wake ambae amekuwa akijitapa kumfukuza chokoraaa kwa kipondo kikali arudi kuimba. Siku hiyo ya jumamosi kutakuwa na mapambano ya ubingwa kati ya Karama nyilawila na Said Mbelwa wakigombea ubingwa wa 
UBO-AFRICA ,wakisindikizwa na kina chokoraa na Abdul manyenza, Suleiman Galile akimkabili Abdala Pazi ‘kiroba’ nae bingwa wa afrika Alan kamote wataoneshana umwamba na Adam ngange, Ramadhan kumbele atazipiga na Hassan kiwale”morobest” , idd athuman na julias kisarawe, nao wababe wa majigambo Zumba kukwe wataoneshana kazi na Kamanda wa makamanda,
 pia kutakuwa na pambano mengine mengi tu ya utangulizi ya mabondia wa tanga watazipiga na mabondia wa dare es salaam. Kama vile Athuman boxa wa tanga atazipiga na waite juma wa chalinze, Rajabu mahoja wa tanga atazipiga na kaisi wa darn a mengineyo yenye kuleta hamasa na burudani za mchezo wa ngumi, kwa vijana kuonesha vipaji vyao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates