REAL Madrid ya Hispania itafanya ziara Tanzania na lini watakuja itajulikana kesho katika Mkutano maalum na Waandishi wa Habari wa kutaja rasmi ziara ya klabu hiyo.
BIN ZUBEIRY inafahamu Kampuni ya 1Plus Communications ya Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi wake, Fina Mango ndiyo waratibu wa ziara hiyo, ambayo hata hivyo itahusisha wachezaji waliowika kwenye klabu hiyo miaka ya nyuma.
Maana yake tutarajie kuwapokea watu kama Ronaldo Lima, Luis Figo, Zinadine Zidane, David Beckham, Roberto Carlos na wengineo.
Magwiji hao wa Real wamekuwa wakifanya ziara za mechi za kirafiki nchi mbalimbali duniani na sasa Tanzania inapata bahati ya kuwapokea nyota wa dunia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni