Social Icons

Ijumaa, 23 Mei 2014

MKATABA WA MIAKA MITATU


 
Hatimaye beki wa kulia wa Arsenal, Bacary Sagna amekamilisha usajili wake Manchester City kwa kupewa mkataba wa miaka mitatu. 



Sagna amemaliza mkataba wake Arsenal, ambapo wakuu wa Emirates walikuwa wakivuta miguu kumpatia mkataba mpya kwa sababu ya umri wake. 

Sagna (31) alikuwa kichocheo kikubwa cha mafanikio Arsenal msimu uliomalizika majuzi lakini Arsenal waliona kwamba umri na fedha alizokuwa akidai vilikuwa juu. 

Inaelezwa kwamba awali alipewa mkataba wa mwaka mmoja Arsenal akakataa, akapewa wa miaka miwili lakini wakashindwana kwenye malipo, akaamua kuondoka.


Alicheza mechi yake ya mwisho kwenye fainali ya Kombe la Ligi wikiendi iliyopita ambapo Arsenal waliibuka na taji baada ya miaka tisa. 


Inaelezwa kwamba mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wamempa mkataba ambao atalipwa pauni 150,000 kwa wiki, ikiwa ni nyongeza kubwa kutoka pauni 80,000 alizokuwa akilipwa Arsenal. 

Hata hivyo, Sagna ambaye kocha Arsene Wenger alijaribu kumbakiza, alikuwa akitaka nyongeza hadi pauni 200,000 na miaka mitatu zaidi hapo Emirates, kiwango ambacho kikilinganishwa na umri wake waliona hakikidhi mahitaji. 

Sagna alikuwa pia akitakiwa kusajiliwa na klabu nyingine kubwa Ulaya kama Paris Saint Germain, na Monaco za Ufaransa na Galatasaray ya Uturuki. 

Kutokana na mazingira hayo, Arsenal wameshaanza mazungumzo kwa ajili ya kumsajili Serge Aurier anayecheza Toulouse ya Ufaransa kuziba nafasi ya Sagna. 

Aurier anayethaminishwa kwa pauni milioni saba amesema wazi kwamba hawezi kukataa ofa kutoka klabu yoyote ya Ligi Kuu England, hata zilizopanda daraja msimu huu kwa sababu ni ligi kubwa. 

Arsenal wameshaanza mazungumzo na klabu yake, ambapo watalazimika kutoa fungu huku Sagna, akiondoka na kusajiliwa bure huko aendako kwa kuwa ni mchezaji huru

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates