Social Icons

Jumanne, 13 Mei 2014

RONALDO KUONGOZA JAHAZI LA URENO KOMBE LA DUNIA, WACHEZAJI 30 WATAJWA KIKOSI CHA AWALI JE NANI ATABAKI NANI ATAENDA BRAZUKA TEGA MACHO YAKO.


article-0-198872C000000578-67_634x386
URENO imetaja kikosi chake cha awali cha wachezaji 30 kwa ajili ya kombe la dunia mwezi ujao nchini Brazil, huku nyota wa Real Madrid na mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo akiongoza jahazi.
Ronaldo na Ureno yake wapo kundi moja na Ujerumani, Marekani na USA na wataanza kampeni zao za kusaka ubingwa dhidi ya Ujerumani juni 16 mwaka huu.
Kocha mkuu Paulo Bento ametaja kikosi cha awali cha wacheza 30 kitakachopunguzwa mpaka kufikia 23 tayari kwa safari ya Brazil.
Ronaldo ameitwa pamoja na nyota wenzake wa Real Madrid, Simon Pepe na Fabio Coentrao.
Wakati huo huo mchezaji wa Porto, Ricardo Quaresma amejumuishwa baada ya kureja katika klabu yake ya zamani mapema msimu huu.

Walinda Mlango: Anthony Lopes (Lyon), Beto (Sevilla), Eduardo (Braga), Rui Patricio (Sporting Lisbon)
Mabeki: Andre Almeida (Benfica), Antunes (Malaga), Bruno Alves (Fenerbahce), Fabio Coentrao (Real Madrid), Joao Pereira (Valencia), Neto (Zenit St Petersburg), Pepe (Real Madrid), Ricardo Costa (Valencia), Rolando (Inter)
Viungo: Andre Gomes (Benfica), Joao Mario (Vitoria), Joao Moutinho (Monaco), Miguel Veloso (Dynamo Kiev), Raul Meireles (Fenerbahce), Ruben Amorim (Benfica), William Carvalho (Sporting Lisbon)
Washambuliaji: Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Eder (Braga), Helder Postiga (Lazio), Hugo Almeida (Besiktas), Ivan Cavaleiro (Benfica), Nani (Manchester United), Rafa (Braga), Quaresma (Porto), Varela (Porto), Vieirinha (Wolfsburg).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates