Wakati tume ya uchanguzi nchini Malawi inataraji kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa Rais nchini humo hivi punde ,zimezuka vurugu kubwa kati ya makundi yanayomuunga mkono Rais Joyce Banda na wapinzani wake.
Imeelezwa kuwa katika vurugu hizo zilizozuka mchana wa leo polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi hao na kumna taarifa ya mtu mmoja kupoteza maisha kutokana na vurugu hizo.
Duru za kisiasa kutoka nchini Malawi zinadai kuwa hali ya amani kwa sasa nchini humu si swari kutokana na vurugu hizo ambapo watu kadhaa wanaripotiwa kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa Hospital kwa matibabu zaidi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni