Social Icons

Jumatano, 28 Mei 2014

MMILIKI WA MAN UNITED AFARIKI DUNIA

 Malcolm Glazer, aliyeshinda tenda ya utata ya kuichukua Manchester United mwaka 2005, amefariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 85.
Mfanyabiashara huyo wa Marekani atakumbukwa kama bilionea wa Florida aliyeichukua kuimiliki binafsi United miaka tisa iliyopita na kuwekeza zaidi ya Pauni Milioni 500. 
Glazer mkubwa amekuwa mgonjwa kwa muda sasa na kuwaachia shughuli za uendeshaji wa United watoto wake wa kiume, Joel na Avram. 
Mmiliki: Malcolm Glazer amefariki akiwa na umri wa miaka 85

Msemaji wa United amesema: "Fikra za kila mmoja katika United zipo kwa familia usiku huu,".
Familia ya Glazer bado wanamiliki Tampa Bay Buccaneers, timu ya mpira wa miguu ya Marekani waliyoinunua mwaka 1995. Na kwenye tovuti ya Bucs, ambako zimetangazwa habari za kifo cha Glazer.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates