Daniel Sturridge akifunga bao lake la kwanza katika dakika ya 32
Kipa wa Peru akijaribu kuokoa shuti la Sturridge bila mafanikio
Steven Gerrard akimpongeza Sturridge baada ya kufunga bao la kuongoza
ENGLAND ilifanya kazi kubwa ya kuvunja ngome imara ya timu ya taifa ya Peru na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mechi ya kimataifa ya kirafiki kujiandaa na kombe la dunia kwenye uwanja wa Wembley mjini London.
England wanaotarajia kuweka kambi yao ya mwisho Miami walipata nguvu kwa bao la kwanza la Daniel Sturridge katika dakika ya 32 na kudumu kipindi kizima cha kwanza.
Mabao mawili ya kipindi cha pili kupitia kwa beki wa kati Gary Cahil na Phil Jagielka yaliweza kuwapa ushinidi wa kwanza baina ya mataifa haya tangu walipokutana miaka 52 iliyopita ambapo ilikuwa ni katika kombe la dunia mwaka 1962 nchini Chile.
Peru walioshindwa kufuzu fainali za kombe la dunia nchini Brazil kutokana na kufanya vibaya katika kampeni za kufuzu katika bara la Marekani kusini, walikuwa na ngome imara ya ulinzi na Jean Deza alisimama vizuri sehemu ya kiungo, huku golikipa wa England Joe Hart akiokoa michumo miwili.
“Ilikuwa ni sherere nzuri ya kutuaga kuelekea kombe la dunia kwa mashabiki wengi kufurika uwanjani”. Alisema kocha wa England, Roy Hodgson wakati akizungumza na ITV.
“Tulitakiwa kuwa wavumilivu kwasababu tulitawala vipindi vyote. Ilikuwa kipimo kizuri wakati huu wiki mbili zikisalia. Nimefurahi kuona mashabiki elfu 85 wamekuja kututakia kila la kheri”.
“Ushindi wa mabao 3-0 ni mafanikio mazuri. Pia ilikuwa kipimo kizuri kwa wachezaji vijana wakati huu wakiaga Wembley”.
Kikosi cha England kilikuwa: Hart, Johnson, Cahill, Jagielka (Smalling 73), Baines (Stones 75), Gerrard (Wilshere 64), Henderson, Lallana (Milner 73), Rooney (Sterling 66), Welbeck, Sturridge (Barkley 82). Subs not used: Foster, Lampard, Lambert, Flanagan, Forster.
Goals: Sturridge 32, Cahill 65, Jagielka 70.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni