Taarifa ya picha kamili za Satelite kuhusu ndege ya Malaysia iliyopotea MH370 zitatolewa kesho kwa mujibu wa maafisa wa nchi hiyo.
Kaimu waziri wa usafirishaji wa Malaysia Hishammuddin Hussein ametoa taarifa kuhusu kutolewa data za ndege hiyo wakati akiwa anatembelea kampuni iliyopo katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur.
Familia na ndugu wa abiria waliokuwemo ndani ya ndege hiyo iliyopotea mwezi Machi mwaka huu ikiwa imebeba watu 239 katika eneo Kusini mwa Asia wamekuwa wakidai data za ajali hiyo kuwekwa hadharani.
Hatma ya waliokuwemo ndani ya ndege hiyo bado imebaki kuwa moja ya kitendawili kikubwa kuwahi kutokea katika nyakati za sasa.
Kampuni ya Inmarsat, ambayo Satelite yake ilikuwa ikiwasiliana na ndege hiyo iliyopotea katika dakika za mwisho imesema kuwa haikupewa kibali na mamlaka za Malaysia kuachia taarifa hizo hadharani.
Lakini sasa kampuni hiyo na serikali ya Malasysia wanasema wanajaribu kufanya taarifa hizo zitolewe hadharani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni