Social Icons

Ijumaa, 23 Mei 2014

Mbatia amlipua Muhongo

  Asema anapingana na sera ya CCM kuwezesha wazawa
  Amtaka aache majivuno na kujisikia
Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, James Mbatia (kulia), akizungumza bungeni mjini Dodoma jana. Kushoto ni Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo. 


Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR-Magezi), James Mbatia, amemlipua Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, kwa kupingana na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayotaka kuwawezesha wazawa.

Aidha, amemshangaa kwa kuwashambulia wabunge wanaozungumzia kuwainua wazawa kiuwekezaji akimkumbusha kuwa ni sera ya CCM kuwawezesha Watanzania kiuchumi na ndiyo maana kuna Mfuko wa Rais maarufu kama Mabilioni ya JK kutimiza azma hiyo.

Akizungumza bungeni jana, Mbatia aliomba mwongozo wa Spika kwa kutumia kanuni 68 (7) na 64 akipinga majibu mabaya na kauli za kumshambulia na kukandamiza alizozitoa Waziri Muhongo wakati akimjibu mbunge huyo swali la nyongeza.

Mbatia alisema kanuni hizo zinaelekeza kuwa katika majadiliano yanayoendelea bungeni hoja zihifadhi uhuru wa kutoa maoni na kuzuia wabunge kutoa taarifa zisizo na ukweli na kutotumia lugha ya kuudhi au inayodhalilisha wengine.

Katika swali la nyongeza, Mbatia alitaka kujua iwapo serikali ina sera za kuwawezesha wachimbaji wa chumvi wa Ikungi, mkoani Singida na Uvinza (Kigoma) ili wawekeze katika madini ambayo ni rasilimali zinazopatikana kwa wingi nchini.

Licha ya swali hilo kuelekezwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri, lilijibiwa na Profesa Muhongo ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini.

Akiomba mwongozo huo, Mbatia alimshangaa Profesa Muhongo kwa kutumia lugha ya kuudhi na kudhalilisha na kusema kuwa ni kinyume cha kanuni hizo.

Mbatia alisema kanuni zinamuagiza Waziri akijibu swali kutotumia lugha ya kuudhi wala kudhalilisha watu wengine, lakini waziri huyo alitumia lugha hizo.

Alisema anamshangaa Waziri kuwa alipouliza swali hakumtaja mtu na kumuonya kuwa kama ana ugomvi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mfuko wa Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi, asiuhamishie bungeni kwani ni suala binafsi.

Baada ya kutoa kauli hiyo, wabunge walipiga makofi kuonyesha kumuunga mkono Mbatia, hatua iliyomlazimisha Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, kuwasihi wasishangilie kwani wanamzuia kusikia hoja.

Mbatia alimweleza Waziri Muhongo kuwa mambo yake dhidi ya kiongozi wa TPSF, hayastahili kuwasilishwa bungeni, kwani haoni kuwa Dk. Mengi ana makosa kwa vile ana haki kama Watanzania wengine ya kuuliza suala lolote.

Alimuonya Muhongo aache kuleta hofu na kuwafanya watu waone kwamba kutaja neno uzawa bungeni na kwingineko ni uhaini na kumkumbusha kuwa katika Ilani ya CCM neno uzawa lipo.

Kadhalika, Mbatia, alimtaka Waziri huyo asilete chuki zake na kusababisha kuondoka kwa amani na utulivu bungeni. 

Mbatia aliyeonekana dhahiri kukasirishwa na kauli za Waziri Muhongo, alimtaka aache majivuno na kujikweza akisema Muhongo aache ‘arogansia’ (arrogance) akimaanisha ana majivuno na kujisikia.

“Ipo sheria ya kuwezesha wazawa wa nchi hii ndiyo maana kuna mabilioni ya JK, kuviwezesha vikundi mbalimbali mbali vya wananchi na Bunge linatenga fedha,” alisema.

Mwenyekiti wa Bunge Zungu, aliahidi kutoa maamuzi ya mwongozo baada ya kutafakari kwa kina kwani suala hilo ni zito. 

MAJIBU YA MUHONGO 
Awali, akijibu swali la Mbatia, Muhongo alisema kuna mtu ambaye iwapo hatapendelewa, basi wazawa hawajasaidiwa licha ya kwamba hakumtaja mtu aliyekuwa akimzungumzia.

Wakati akijibu swali hilo alimfokea Mbatia akimwambia….”Sikiliza si umeuliza madini ….”

Alijibu kuwa jitihada za kuwawezesha wazawa wizara hiyo imetenga fedha za kuwasaidia wachimbaji wadogo wanazokopeshwa kupitia Benki ya Rasilimali (TIB) na kwamba kila kikundi kinapewa Dola za Marekani 50,000.

Alisema katika vikundi vilivyokopeshwa vipo vya wanaochimba chum

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates