Social Icons

Ijumaa, 30 Mei 2014

WABUNGE WA KAMBI RASMI YA UPINZANI WASUSIA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI NA KUTOKA NJE YA BUNGE


Kiongozi  wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe amewatoa wabunge wote wa upinzani Bungeni ikiwa ni shinikizo la kuipinga Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kama ilivyokuwa imewasilishwa na Waziri wa Wizara hiyo Professa Sospeter Muhongo.

 
"Hatuwezi kuendelea kuzungumzia bajeti ya Serikali isiyokuwa na sera,mimi kama Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni siwezi kuendelea kuiongoza kambi inayoburuzwa," amesema Mbowe na kuongeza:
 
"Tunawaachia bungeni lenu mpitishe bajeti yenu ili siku zijazo mkutane na hasira za wananchi,kwakuwa haya mlishayapanga".

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates