Nyota wa Liverpool, Luis Suarez ameongeza tuzo katika orodha yake ya tuzo, baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji Bora wa Msimu wa 2013/2014 wa Ligi Kuu soka nchini England.
Suarez amefumania nyavu mara 31 na kutoa pasi 12 za mabao katika mechi 33 za Ligi Kuu alizocheza, huku timu yake ya Liverpool ikizidiwa na Manchester City kwenye mbio za ubingwa.
Suarez, ambaye pia ameshinda tuzo ya mchezaji Bora wa Wachezaji wa PFA na Mchezaji Bora wa Waandishi wa habari za Soka msimu huu, alinyakua tuzo ya nne msimu huh baada ya Kiatu cha Dhahabu cha Ligi.
Mpachika mabao huyo wa Uruguay, ambaye anajiandaa kukutana na England katika Fainali za Kombe la Dunia Juni 19, alimaliza msimu akiwa mfungaji bora- akimzidi kwa mabao 10 mchezaji mwenzake wa Wekundu hao, Daniel Sturridge.
Brendan Rodgers ameshinda tuzo ya kocha bora kuliko wote nchini England. |
Tuzo hiyo maarufu kama LMA hutolewa baada ya makocha katika madaraja yote nchini humo kupiga kura kumchagua nani ni bora zaidi.
Pamoja na Liverpool kushika nafasi ya pili lakini Rodgers amekuwa kocha wa Liverpool kushinda tuzo hiyo.
Wakati kocha huyo wa Liverpool akibeba tuzo hiyo ya juu zaidi, Tony Pulls wa Crystal Palace amekuwa kocha bora wa Ligi Kuu England.
Hii maana yake, Rodgers ni bora kwa England kwa kujumuisha na ligi zote ikiwemo Ligi Kuu England wakati Pulls ni kocha wa ligi hiyo moja tu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni