Kocha Arsene Wenger amerudia tena juhudi zake za kutaka kumsajili Mfaransa mwenzake, Karim Benzema.
Benzema amebakiza mkataba wa miezi 12 na Real Madrid.
Wenger amekuwa akifanya kila juhudi kumpata Benzema tokea akiwa Lyon ya kwao Ufaransa
kabla ya kujiunga na Real Madrid.
Lakini ameanza tena harakati hizo baada ya kusikia Kocha wa Madrid, Carlo Ancelotti ana
mpango wa kumsajili Luis Suarez.
Hivyo itakuwa ni nafasi nzuri kwa Benzema kung’oka Madrid, Wenger anaamini Mfaransa huyo ni chakuo sahihi kwa kikosi chake msimu ujao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni