KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Croatia , Niko Kovac ametangaza kikosi cha awali kwa ajili ya kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil, huku nyota wakiwa ni Luka Modric na Mario Mandzukic .
Kocha huyo mwenye miaka 42 amemjumuisha mlinda mlango, Oliver Zelenika, mshambuliaji Duje Cop, viungo Marcelo Brozovic, Ivan Mocinic na Mario Pasalic katika kikosi chake cha awali cha wachezaji 30.
Nikola Kalinic ambaye amefunga mabao 22 katika mechi 32 alizoichezea klabu yake ya Dinamo Zagreb msimu huu ametuwa nje.
Walinda Mlango: Stipe Pletikosa (Rostov), Danijel Subasic (Monaco), Oliver Zelenika (Lokomotiva).
Walinzi: Igor Bubnjic (Udinese), Vedran Corluka (Lokomotiv), Dejan Lovren (Southampton), Danijel Pranjic (Panathinaikos), Gordon Schildenfeld (Panathinaikos), Darijo Srna (Shakhtar), Ivan Strinic (Dnipro), Domagoj Vida (Dynamo Kyiv), Sime Vrsaljko (Genoa).
Viungo: Marcelo Brozovic (Dinamo), Milan Badelj (Hamburg), Mateo Kovacic (Inter), Niko Kranjcar (QPR), Ivan Mocinic (Rijeka), Luka Modric (Real Madrid), Mario Pasalic (Hadjuk), Ivan Rakitic (Sevilla), Jorge Sammir Cruz Campos (Getafe), Ognjen Vukojevic (Dynamo Kyiv)
Washambuliaji: Duje Cop (Dinamo), Eduardo (Shakhtar), Ivo Ilicevic (Hamburg), Nikica Jelavic (Hull City), Mario Mandzukic (Bayern Munich), Ivica Olic (Wolfsburg), Ivan Perisic (Wolfsburg), Ante Rebic (Fiorentina)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni