Social Icons

Jumamosi, 31 Mei 2014

MBEYA; MUME AUA MKE KIKATILI



MWANAMKE aliyetambuliwa kwa jina la Christina Hayola(35), mkazi wa Kijiji cha Lwalanje, alikutwa amekufa na mwili wake kubainika kuwa ulikuwa na majeraha ya kukatwa katwa Kifuani, kichwani na mguu wake wa kulia.
 
Unyama huo unadaiwa kufanywa na mumewe, Mussa Nsagaje, maarufu kwa jina la Mwaulambo, kwa kile kinachodaiwa kuwa chanzo ni ugomvi wa masuala ya wivu wa kimahusiano(Ngono) ulioanzia eneo la kilabu cha pombe.
 
Mwili wa marehemu ulikutwa katika Kijiji cha Magamba, kata ya Isansa, tarafa ya Igamba, wilayani Mbozi, mkoani Mbeya na mtuhumiwa alitoroka baada ya kutekeleza mauaji hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates