Social Icons

Ijumaa, 16 Mei 2014

Upinzani watikisa,Chama cha Congress chashindwa India.

Baada ya kutawala kwa miaka kumi, chama cha Congress kimekubali kushindwa katika Uchaguzi Mkuu nchini humo.

Kiongozi wa BJP, Narendra Modi, anayetarajiwa kutangazwa kuwa Waziri Mkuu wa India.
Kura ambazo zimehesabiwa kufikia sasa zinaonyesha kuwa muungano wa vyama unaoongozwa na chama BJP, chini ya Bwana Narendra Modi, utashinda kwa wingi wa kura.
Tayari shangwe, vifijo na nderemo vinaonekana na kusikika katika makao makuu ya BJP huku wanachama wakicheza densi barabarani na fataki kulipuliwa.
Tume ya Uchaguzi ya India imesema kuwa matokeo ya awali yanathibitisha kuwa BJP kimeshinda viti 272, vinavyokiwezesha kutawala bila kushirikiana na chama kingine.
Zaidi ya watu milioni 500 walipiga kura ambayo ni asilimia 66 ya wote waliochaguliwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates