Social Icons

Jumatatu, 28 Aprili 2014

Jeshi la Uganda lamkamata kamanda wa kundi la L.R.A

Kundi hilo la waasi wa Uganda linafahamika kwa kushambulia na kufanya wizi wa ngawira katika vijiji na kulazimisha watoto kujiunga nalo kama wapiganaji.

Joseph Kony, kiongozi wa kundi la waasi wa Uganda, L.R.A.
Jeshi la Uganda linasema majeshi  yake yamemkamata kamanda mmoja wa kundi la waasi la Lord’s Resistance Army ( L.R.A.) Charles Okello na kuwaachia  wengine 10 ambao walishikiliwa mateka na kundi hilo la waasi.

Haya ni kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Uganda anayesema kukamatwa kwake kulifuatia kuzingirwa kwa kundi hilo katika  maficho yao huko  Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kundi hilo la waasi wa Uganda  linafahamika kwa kushambulia na kufanya wizi wa ngawira katika vijiji na kulazimisha  watoto kujiunga nalo kama wapiganaji.

Liliundwa kati kati ya miaka ya 1980 na lilipambana na serikali ya Uganda kwa miaka 20 kabla kukimbilia nchi jirani.
 
Majeshi ya Uganda yamekuwa yakiongoza operesheni za Umoja wa Afrika zinazoungwa mkono na Marekani ili kumkamata kiongozi wa kundi hilo, Joseph Kony na viongozi wengine .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates