Social Icons

Jumapili, 20 Aprili 2014

ROONEY NA FELLAINI WAPO TAYARI KUIVAA EVERTON


rooney_16d65.jpg

Kocha Manchester United (David Moyes) amesema kuwa Wayne Rooney na Marouane Fellaini watakwepo katika kikosi cha kwanza kitakachokumbana na Everton siku ya Jumaapili, akiitaja miamba ya mashetani wekundu itaowavaa Everton, Moyes aliwataja Rooney na Fellaini kuwa ni miongoni mwa wachezaji watakaocheza katika mtanange huo.
Fellaini ambaye alikosa mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya katika hatua ya robo fainali dhidi ya Bayern Munich atakuwa fiti kukumbana na Everton wakati Wayne Rooney nae yupo tayari kuibeba ngao ya Man United tayari kupigania ushindi.
Wayne Rooney alishindwa kuonesha makali yake katika mtanange wa klabu bingwa ulaya dhidi ya Bayern Munich baada yakutandikwa mabao 3-1, Rooney aliulimia katika mchezo huo lakini mpaka sasa, Mshambuliaji huyo wa Manchester United yupo tayari kupambana na Everton katika dimba la Goodison Park.
Moyes alisema kuwa Rooney yupo ngangari kwa sasa kwani amefanya mazoezi ya kutosha kwa wiki zima, hivyo atakwepo katika kikosi hicho kitakacho vaana na Everton siku ya jumaapili.
Mskotishi huyo (David Moyes), aliwataja wachezaji ambao bado nimajeruhi kuwa ni Rafael na Rob Van Persie ambao wataukosa mtanange huo wakati akiwataja majeruhi hao, kocha huyo alionesha kuwapa moyo mashabiki wa timu hiyo baada ya kutoa taarifa ya John Evans kuwa atakwepo katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates