Social Icons

Jumatano, 30 Aprili 2014

TAZAMA PICHA- MKUTANO WA UKAWA KATIKA VIWANJA VYA KIBANDA MAITI MJINI UNGUJA, ZANZIBAR JANA


Viongozi wa Wajumbe wa kundi la UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi) ndani ya Bunge Malaum la Katiba, wamehutubia maelfu ya watu waliohudhuria mkutano wao katika viwanja vya Kibanda Maiti mjini Unguja, Zanzibar jioni ya leo.
 

Kwa mujibu wa Katibu wa UKAWA ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, kesho mkutano mwingine wa UKAWA unatarajiwa kufanyika Pemba kabla ya mikutano kama hiyo kuendelea katika baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara/Tanganyika kama vile Dar es Salaam, Kigoma, Morogoro, Mwanza, Iringa, Arusha n.k. 

Mtatiro amesema lengo la mikutano hiyo ni kuwaelimisha wananchi juu ya hatua yao ya kuondoka Bungeni na kususia vikao vya Bunge Maalum la Katiba na kile wanachoamini kinapaswa kufanyika.
 
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates