Social Icons

Jumanne, 22 Aprili 2014

BREAKING NEWS: MAN UNITED YATHIBITISHA KUMTIMUA KAZI MOYES – GIGGS KUSHIKA HATAMU

Hatimaye kocha Manchester United David Moyes amefukuzwa kazi, miezi 10 baada ya kumrithi Sir Alex Ferguson.

United jana waligoma kuthibitisha kuhusu ripoti kwamba Moyes angefukuzwa mwishoni mwa msimu.
Moyes, 50, alichaguliwa na Sir Alex Ferguson kumrithi wakati kocha huyo mwenye 72, alipoamua kustaafu baada ya miaka 26 mwaka jana baada ya ligi kuisha.
Moyes aliondoka Everton na kusaini mkataba wa miaka sita na mabingwa ya Premier league.
Kwenye taarifa rasmi, klabu ilisema: “Tungependa kumshukuru kwa kazi nzuri aliyoifanya, uaminifu wake aliokuwa nao kwenye kazi yake”.
Ryan Giggs kwa pamoja na Nicky Butt watashika majukumu ya ukocha mpaka mwishoni mwa msimu.
1560414_715196531877628_3796186308205047484_n

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates