Social Icons

Jumatano, 30 Aprili 2014

Yule tajiri Mmarekani aliesema hataki watu Weusi kapewa hii adhabu

Screen Shot 2014-04-30 at 3.30.29 AM
NBA imesema kutokana na uchunguzi kukamilika kuhusu mmiliki wa timu ya Los Angeles Clippers Donald Sterling dhidi ya maneno ya kibaguzi kwa watu weusi, imempa kifungo cha maisha mmiliki huyo mwenye umri wa miaka 80.

Wanasema baada ya kufanya uchunguzi Donald amekubali kwamba sauti iliyosikika ikitoa maneno mazito ya kibaguzi dhidi ya watu weusi ni ya kwake ambapo alikua akiongea na Mwanamke anaedaiwa kuwa mpenzi wake.
Donald ambae aliwahi kukiri siku kadhaa zilizopita kwamba hatoiuza hii timu, kwenye adhabu ya maisha aliyopewa ni kwamba hatoruhusiwa kuhudhuria mazoezi ya timu yake wala kwenda kwenye game zote maishani mwake na vilevile hatoruhusiwa kufanya maamuzi yoyote kwenye timu.
Screen Shot 2014-04-30 at 3.35.06 AM
Kingine kilichoongezeka ni faini ya dola za Kimarekani milioni 2.5 ambazo kibongobongo inagonga kwenye 4107500000 ambapo inasemekama hii sauti ya Sterling akitoa maneno ya kibaguzi ilirekodiwa September 2013 na kwamba alishtukia kwamba karekodiwa.

Yote haya yametokana na kuvuja kwa sauti ya mazungumzo kati yake na girlfriend ambapo Donald Sterling aliongea maneno makali ya kibaguzi kwa kusema kwamba hataki girlfriend wake ajihusishe na watu weusi kwa kupiga picha au kwenda nao kwenye mechi.
Imeshangaza zaidi kwa sababu timu yake ina wachezaji mashuhuri weusi kama Chris Paul na Blake Griffin aliyewahi kucheza ligi ya chuo pamoja na Mtanzania Hasheem Thabeet lakini wakiwa wanatoka kwenye vyuo tofauti.
Kamishna wa NBA amesema atatumia nguvu ya uongozi wake kuhakikisha L.A Clippers haimilikiwi tena na Donald Sterling.

Screen Shot 2014-04-30 at 3.27.39 AMScreen Shot 2014-04-30 at 3.27.31 AM

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates