Social Icons

Ijumaa, 2 Mei 2014

NDITI AIONGOZA CHELSEA KUITWANGA MAN CITY MBELE YA KOCHA WAO VIERA.


NDITI AKIWA KAZINI HIYO JANA
Adam Nditi ameiongoza timu yake ya Chelsea chini ya miaka 21 kuifunga Man City kwa mikwaju ya penalti katika mechi ya Ligi Kuu ya Vijana England chini ya miaka 21, jana.


Nditi ambaye asili yake ni Tanzania alicheza kama beki wa kati na kwa dakika 120 timu hizo zikamaliza kwa sare ya mabao 1-1.
 
AKISHANGILIA NA WENZAKE
Chelsea walianza kupata bao katika dakika ya 14 kupitia Islam Feruz mwenye asili ya Tanzania pia, lakini City wakasawazisha zikiwa zimebaki dakika 14 mpira kwisha kupitia Olivier Ntcham.

Ntcham ndiye aliyekosa mkwaju wa penalti ambao uliisaidia Chelsea kusonga mbele na huenda ikakutana na kati ya Liverpool au Manchester United katika kampeni zake za kutwaa ubingwa wa England kwa U-21.
 
VIEIRA AKISHANGILIA NA WACHEZAJI WAKE BAADA YA KUSAWAZISHA
Patrick Vieira ambaye ni kocha wa timu hiyo ya vijana ya Man City, alimshuhudia Nditi akionyesha mambo yake na kuwazuia mafowadi wake kupata bao la ziada.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates