Social Icons

Alhamisi, 8 Mei 2014

NADIR HAROUB, NAHODHA MPYA, KWENYE MATARAJIO MAPYA…


CANNA
Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mholanzi, Martin Nooij amempatia nafasi ya jukumu la Unahodha wa kikosi hicho mlinzi wa kati, Nadir Haroub, huku mlinzi mwingine wakati, Aggrey Morris akiwa kaimu nahodha wa timu hiyo ambayo itacheza na timu ya Zimbabwe katika michezo miwili ya mtoano kuwania kufuzu katika hatua ya makundi kuwania nafasi ya kufuzu kwa michuano ya AFCON 2015, Nchini, Morocco.
Nadir amejiimarisha na kuwa mchezaji bora kwa mara nyingine baada ya kuanza msimu uliopita kwa kusuasua, amesisimua kwa uchezaji wake katika raundi ya pili ya ligi kuu Tanzania, na kitendo cha kurudishwa ghafla kikosini, Stars kinaweza kutoa wazo mbadala kwa makocha wapya, Nooij, na Salum Mayanga katika wazo mbadala la kuunda upya safu ya ulinzi wakati katika mechi hizo muhimu kwa timu ya Tanzania..
Katika michezo miwili dhidi ya Al Ahly, Nadir, alicheza kwa kiwango kilichostahili kiasi cha kukumbusha enzi zake akiwa roho ya safu ya ulinzi ya Stars chini, Marcio Maximo.
Alikuwa bora katika michezo yote miwili ya klabu yake dhidi ya waliokuwa mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri katika michuano ya klabu bingwa, sawa na alivyocheza katika ligi kuu, raundi yapili. Kama alimudu kucheza vizuri mechi ya Afrika iliyoshirikisha klabu bora, anastahili kuvaa jezi ya Stars dhidi ya Zimbabwe. 
Tanzania haina uhakika kama itawaondoa, Zimbabwe, timu hiyo inawashambuliaji wakali. Tofauti na ilivyokuja, novemba, 2013, katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki,safari hii, Zimbabwe itakuja, Tanzania na kikosi cha kupambana huku, Knowledge Musona akiongoza safu ya mashambulizi. Wachezaji, Nadir, Aggrey, Said Mourad, Kevin Yondani wanatosha katika nafasi ya ulinzi wa kati. Awali, Nadir alitemwa kwa sababu za kisoka, na sasa ni sababu hizo hizo zimemrejesha na kumpatia ‘ beji ya unahodha’. Beki huyo aliyeiwakilisha, Tanzania katika michezo 35 na kuifungia goli moja, alipangwa pamoja na Aggrey katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Malawi, siku ya jumapili iliyopita na walicheza vizuri.
Nadir, amepevuka vya kutosha kwasasa katika mchezo wake. Safu ya ulinzi ya Stars chini ya Shomari Kapombe, Nadir, Aggrey na ErastoNyoni, ilifanya kazi nzuri kwa dakika zote dhidi ya Malawi katika mchezo uliomalizika kwa suluhu-tasa, kuliko vile walivyocheza na Burundi na kuchapwa magoli 3-0, siku kumi zilizopita. Walijipanga vizuri, walikuwa imara na hawakutoa nafasi kwa washambuliaji wa Malawi. Stars ilikuwa imara katika ulinzi kutokana na uwezo wa mabeki wa kati na wale wa pembeni. 
Kurejeshwa kundini kwa Yondan ni jambo zuri kwa kuwa mlinzi huyo ana uzoefu wa kutosha. Nooij, anaweza kufanikiwa katika malengo yake ya kuipaisha, Stars kama wachezaji wazoefu waliopo watajitoa kwa timu.
Zimbabwe ni timu, si ngeni kwa wachezaji wa Stars, hivyo wanatakiwa kupokea mafunzo ya walimu wao kwa uhakika ili kuweza kufuzu katika kundi la tano, ambalo tayari timu za Zambia, Cape Verde na Niger zimefuzu moja kwa moja. Nahodha huyo mpya wa Stars ameonekana kuhamasika na jukumu hilo

Kama, wachezaji wazoefu watacheza kwa kiwango kizuri timu itanufaika na uzoefu wao, ila endapo wataendelea kucheza kwa viwango vilevile vya siku zote. Hakutakuwa na kipya katika timu hiyo na Nooij ataanguka kama walivyoondoka, Marcio Maximo, Jan Poulsenna KIM. Japokuwa tumewalaumu makocha wote waliopita, kuwa hawakuwa na mbinu nzuri za kuipandisha Stars, ukweli walijitahidi lakini wakaangushwa na baadhi ya wachezaji muhimu ambao waliwekeza mbinu zao kwao. Nooij, amejipa mwenyewe alama ya mapinduzi, Malinzi amesema kuwa hakuna mtu atakayemuingilia katika uteuzi wa wachezaji, sasa nijukumu la wachezaji kuamua na kuamini wanaweza kufuzu kwa fainali za Afrika.
Siku 13 kabla ya kuivaa, Zimbabwe, kocha wa Stars, Nooij alisifu namna timu yake ilivyoweka mpira chini dhidi ya Malawi, ila amelalamikia upotezaji wa nafasi za kufunga ambazo wachezaji wake walizipoteza katika mchezo huo.Chini ya mwalimu, Maximo, Stars ilikuwa ngumu kufungika, ukitoa kipigo cha Dakar, Stars haikufungwa magoli zaidi ya mawili katika mechi moja katika michezo ya mashindano. Maximo alipata bahati ya kufanya kazi na wachezaji wenye nidhamu kubwa, ShadrackNsajigwa, Mecky Mexime, Salum Sued, Nadir, Erasto Nyoni, na Victor Costa. Hawa ndiyo walinzi walioifanya Stars kuwa ngumu kufungika chini ya Maximo, walikuwa wakicheza kwa kujituma na nidhamu, walisumbuliwa na tatizo la kukosa umakini ila usingeweza kufunga magoli matatu. Alipokuja, Jan, kisha KIM, Stars imekuwa ikifunguka na kucheza kwa kushambulia zaidi. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates