Mmarekani huyo akiwa na kibegi kidogo chenye saa 18 aliandika maneno yafuatayo: ” @thatjessilee na @badmedina wanacheza mchezo, kuona nani anaweza kuhesabu dola laki moja ( $100,0000) kwa haraka zaidi. Hivi ndivyo wanafanya wakichoka. #TheMoneyTeam #FollowBeautifulLadies’.
Ni haki yake kusema dola laki moja ni fedha kidogo kwa bondia huyo bingwa mara tano wa dunia, ambaye alipata dola milioni 70 kutokana na pambano lake dhidi ya Maidana.
Alipata dola milioni 32 kenye mchezo uliopigwa MGM Grand , na vilevile anasema anapata dola milioni 38 kutokana na matangazo ya televisheni.
Wanawake wawili, Jessi Lee na Doralie Medina walipigwa picha wakiwa kama sehemu ya wasaidizi wa timu ya Mayweather, inayojulikana kama Timu ya hela ` The Money Team (TMT)`.
Medina, akionekana amepumzika. Hii picha ipo katika akaunti yake ya Instagram
Msichana mwingine aliyeshindana kuhesabu pesa za Mayweather ni Jessi Lee
Mapambo: Nyota wa masumbwi, Floyd Mayweather alionesha picha yake ya vito vyake Instagram mwezi uliopita
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni