Social Icons

Alhamisi, 8 Mei 2014

MANCHESTER UNITED YATUPWA VILABAU TAJILI DUNIANI.

forbesforbesmost-valuble-soccer-teams
Klabu ya Manchester United imezidi kushuka chini kwenye chati ya vilabu vyenye thamani kubwa ulimwenguni, kwa mujibu wa jarida la Forbes.

Nafasi ya kwanza imeshikwa na klabu ya Real Madrid yenye thamani ya £2billion, nafasi ya pili FC Barcelona ambayo imetajwa kuwa na thamani ya £1.9billion.
United baada ya kuwa msimu mbaya kabisa kwenye historia yao, wameshuka kutoka nafasi ya 2 mwaka jana mpaka nafasi ya 3 wakiwa na thamani ya £1.65billion.
Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wameshika nafasi ya nne kwa kuwa na thamani ya £1.1billion, wakati huo huo klabu ya Manchester City imeweza kupanda thamani kwa asilimia 25 wakiwa na thamani ya  £508m.


984068_237972503058041_3057865779243803531_n


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates