Msururu wa magari ukiwa mkubwa katika eneo hilo baada ya kushindwa kupita kutokana na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka.
Wananchi na wasafiri mbalimbali wakitoka kuangalia tukio hilo.
Askari wa usalama barabarani akihakikisha mambo yanakwenda sawa na usalama unaimarishwa katika eneo hilo.
****
Tanki la mafuta la kampuni ya B. Clarke Haulege Construction limelipuka na kuwaka moto maeneo ya Shelui mkoani Singida na kusababisha adha kubwa kwa wasarifi....
Tanki hilo, mali ya Bw. Bundala Kapela wa Igunga lenye namba T634 BCZ, vyumba vinne na uwezo wa kubeba lita 40.000 za mafuta ya Petroli lililipuka majira ya Saa 11:00 katika barabara kuu ya Dodoma - Mwanza eneo la Shelui mkoani Singida wakati breki za tanki hilo upande wa kushoto zilipojam na kusababisha moto....
Sakata hilo lilimfanya dereva wa roli lenye namba za usajiri T164 CGF aina ya Scania lililokuwa likivuta tanki hilo kusimamisha na kukata haraka tanki hilo huku akiondoa haraka injini ili kuepusha madhara zaidi ambayo yangeweza kutokea....
Ajali hiyo ilisababisha usumbufu mkubwa kwa abiria na msururu wa magari kushindwa kupita katika eneo hilo kutokana na moto mkubwa uliochanganyika na moshi kutishia usalama wa watumiaji wengine...
Hata hivyo baada ya moto kupungua, askari wa usalama barabarani waliamuru magari yaanze kupitia pembeni mwa barabara hiyo ili kuendelea na safari
Hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika ajali hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni