WAYNE Rooney anahitaji kuwa nahodha wa Manchester United kuelekea kusaka ubingwa, lakini amesisitiza kuwa ataheshimu maamuzi ya kocha mkuu Louis Van Gaal kwa yeyote atakayemchagua.
Robin Van Persie anatajwa kuchaguliwa kuwa nahodha wa United kutokana na mahusiano mazuri aliyonayo na kocha Van Gaal kuanzia timu ya taifa ya Uholanzi.
Wakati huo huo Darren Fletcher alivaa kitambaa cha unanodha katika ushindi wa 7-0 dhidi ya La Galaxy alhamisi ya wiki hii.
Rooney ana imani kuwa Man United itafuta makosa ya msimu uliopita chini ya kocha Van Gaal ambapo ilimaliza katika nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi kuu soka nchini England.
“Kiukweli tunaweza kushinda ubingwa,” aliwaambia waandishi wa habari. “Msimu uliopita tulikuwa wabaya sana, tunajua hilo, lakini tuna imani tutafanya vizuri. Tunatakiwa kuamini kuwa tunaweza kutwaa ubingwa”.
“Sio siri, ningetamani kuwa nahodha, lakini ni maamuzi ya kocha kuchagua anayemtaka. Anahitaji kufanya kazi na wachezaji na kuchagua nahodha kutoka kwa wachezaji hao”.
“Sidhani kama anaweza kutoka nje na kuchagua nahodha. Nina uhakika atachagua miongoni mwa wachezaji walioopo na kufikia maamuzi wiki zijazo”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni