Social Icons

Jumanne, 15 Julai 2014

MAPOKEZI YA TIMU YA ARGENTINA YASISIMUA

Timu ya taifa ya Arggentina imepokelewa kwa shangwe na maelfu ya watu waliotaka kuwapongeza wachezaji wao, kuanzia uwanja wa ndege. Wanandinga hao walishuka kutoka kwenye ndege maalum iliyokuwa imenakshiwa kwa rangi za timu hiyo ikiwa na maandishi yaliyomaanisha 'Asante Argentina' kwa lugha ya kwao.

Wachezaji hao walipita kwenye mitaa wakiwa ndani ya mabasi maalum huku kukiwa na mapokezi makubwa kuwahi kushuhudiwa.
Argentina iliingia fainali za kombe la Dunia 2014, na kushindwa kutimiza ndoto yao ya kutwaa kombe hilo kwa kufungwa na timu ya Ujerumani kwa bao moja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates