Maelfu ya mashabiki wa soka wamekuwa wakisubiri tangu asubuhi na mapema mjini Berlin kuwakaribisha wachezaji hao.
wa dada wakiwa wamevaa flana zenye nembo ya Dr.dree(beats) baada ya dree kutoa head phone za dhabu kwa timu ya ujerumani.
Sherehe zitafanyika katika eneo la Brandenburg Gate, ambako wachezaji wataonyeshea kombe lao, ambalo walilishinda katika fainali ya mashindano hayo dhidi ya Argentina.
Shangwe na vigelegele vimeshuhudiwa huku umati mkubwa wa watu ukitarajiwa kushuhudia kombe hilo ambalo litapitishwa mjini kote.
Watu wengi wamenunua jesi zenye nyota nne kuashiria ushindi wa nne wa nchi hiyo katika kombe la dunia.
Wachezaji wa timu hiyo ambao huchezea timu ya Bayern Munich pia watapata ukaribisho mkubwa baadaye mjni Munich.
Mwandishi wa BBC Steve Evans ambaye yuko mjini Berlin anasema kuwa watu nusu milioni wanatarajiwa kukutana na wachezaji hao mjini Berlin.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni