Muigizaji na Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha E! cha nchini Marekani, Terrence J akiongea mbele ya wasanii fani mbalimbali kutoka Tanzania leo.
Baadhi ya wadau wa Sanaa wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Wasanii wa Muziki na Filamu kutoka Nchini Marekani ambao wameendesha warsha kwa wasanii wa bongo
Izzo Business akiwa makini
Wadau wa sanaa kutoka nchini Tanzania wakifuatilia mada kwa makini
WASANII mbalimbali na wadau wa sanaa nchini Tanzania leo wamepewa semina ya jinsi wanavyoweza kuanzisha soko thabiti la kazi zao kwa kuiga mfumo wa nchi ya Marekani.
Semina hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Bank Kuu ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wasanii wa Bongo Fleva, Maigizo, Muziki wa Injili, Maprodyuza na wadau mbalimbali wa tasnia hiyo huku wageni waalikwa wakiwa ni Aliyekuwa meneja wa msanii wa muziki Ludacris na Prodyuza, Shaka Zulu. Mwana Hiphop na Prodyuza, David Banner na Terrence J ambaye ni staa wa Think Like A Man 2, mwingine ni Liver Sheldon
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni