Social Icons

Jumamosi, 26 Julai 2014

ADAM LALLANA WA LIVERPOOL KUKOSA MECHI MWANZONI MWA LIGI

Adam Lallana to miss start of season
Timu ya Liverpool imethibitisha leo mchezaji wao kiungo Adam Lallana waliomsajili kutoka Southampon mapema mwezi huu atakosa kucheza mechi za kwanza kwenye ligi ya Uingereza kutokana na maumivu ya goti.

Adam Lallana alipata maumivu wakati akifanya mazoezi kwenye Red's Harvard University iliyopo mji wa Boston, Massachusetts nchini Marekani.

Adam Lallana ameishachekiwa na madaktari wa timu ambao wamesema goti lake halihitaji upasuaji na hakuna muda uliowekwa kwa Adam Lallana kurejea uwanjani lakini majeruhi kama yeye huchukua mpaka wiki sita kuwa fiti.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates