Social Icons

Jumatano, 2 Julai 2014

Ajali ya ndege yawaua wanne Kenya leo.

Ajali ya ndege Nairobi

Shughuli za uokozi zikiendelea baada ya ndege ya mizigo kuanguka jijini Nairobi
Watu wanne akiwemo Rubani wa ndege moja ya mizigo, wamefariki dunia baada ya ndege walimokuwa kuanguka mapema leo asubuhi katika mtaa wa Embakasi jijini Nairobi.
Kwa mjibu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya, ndege hiyo ilianguka dakika chache tu baada ya kuruka kutoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Ndege hiyo ya mizigo ilikuwa imebeba shehena ya Miraa ama Mairungi kuelekea Mogadishu nchini Somalia.
Uchunguzi umeonyesha kuwa ndege hiyo huenda iligonga mlingoti wa stima karibu na mtaa wa Embakasi, mjini Nairobi na kuanguka.Screen Shot 2014-07-02 at 08.25.08

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates