Social Icons

Jumapili, 27 Julai 2014

MKUU WA MKOA MOROGORO AONGOZA MAMIA KUMZIKA MKE WA MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO KUSINI.



Mkuu wa mkoa akimpeleka Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh  Innocent Kalogeris  kupokea mwili wa mpendwa mke wake,kulia ni dada wa mbunge huyo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Dr Joel Bendera Leo amewaongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Morogoro kumzika Mke wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini, Mh lnocenti Kalogeris watu mbali mbali wakiwemo wabunge,wakuu wa mikoa wa staafu na watu mashuhuri wamefurika nyumbani kwa mbunge huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro CCM 


 Marehemu Elizabeth Kapoloma enzi za Uhai wake , Bi,Elizabeth Kapoloma alifariki Alhamisi Kwa Ugonjwa Moyo.
 Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani kwake kwajili ya Heshima za Mwisho na Ibada kabla ya Mazishi leo


                       

  Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh Dk Joel Bendera akimbembeleza Mume wa marehemu Mhe lnocent Kalogeris
 Mbunge huyo akiingizwa kwenye chumba kilichowekwa jeneza lenye mwili wa mpendwa mkewake.

 Diwani wa Kata ya Mji Mpya Wensilaus Karogerezi ambaye ni kaka wa mbunge huyo akiangua kilio kwa uchungu baada ya kuondokewa na mpendwa shemeji yake
 Mstakihi Meya wa Mji wa Morogoro Amir Juma Nondo ambaye pia ni Diwani wa kata ya Boma akimbembeleza Diwani mwenzake  Wensly Kalogeris  Ambaye Pia ni Kaka wa Mbunge wa Jimbo ala Morogoro Kusini
 Mtoto wa Marehemu akiangua kilio baada ya mwili wa mpendwa mama wake kuwasili nyumbani kwao 




                 Mbunge wa viti maalumu'CCM'  Mhe Magreth Mkanga

 Mbunge mstaafu wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Lotto akimpa pole Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh lnnocent Kalogeris Kwenye mazishi ya Mkew a Mbunge Huyo.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro  Mhe  lnnocent Kalogeris akifarijiana na mama yake mzazi 

Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates