Heshima: Gwiji wa Manchester United akipozi katika picha baada ya kupata digrii yake kwenye ukumbi wa Victoria Hall mjini Bolton.
GWIJI wa Manchester United, amezawadia shahada ya heshima ya Udaktari na chuo kikuu cha Bolton kutokana na mchango wake mkubwa aliotoa katika mchezo soka.
Giggs aliyestaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu uliopita amepokea udaktari wa sayansi kwa mchango wake mkubwa katika michezo kwenye mahafali ya chuo iliyofanyika ukumbi wa Victoria Hall mjini Bolton jana ijumaa mchana.
Giggs anaongeza shahada hiyo katika shahada yake ya kwanza ya OBE aliyopata kutoka kwa Malkia mwaka 2007, shahada ya pili (MA) alipewa mwaka uliofuata na chuo cha Salford.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni