Na Andrew Chale, Chamwino, Dodoma
Tamasha la saba la Muziki wa Cigogo 2014, lililoanza jana Julai 25, kwenye kijiji cha Chamwino Ikulu, Mkoani hapa linarindima kwa kishindo na kufanya nji wote kuwa na shamrashara za aina yake.
Tamasha hilo ambapo jana lilizinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, linashirikisha vikundi zaidi ya 30 vikiwasha moto wa ngoma na muziki wa kitamaduni.
Kwa mwaka huu tamasha hilo ni la msimu wa Saba (7) likifahamika kama (Wagogo music festival 2014) lenye kauli mbiu ‘Utamaduni na Amani’ linarindima kwa siku tatu na hiyo kesho Julai 27 linatarajia kufikia tamati.
Mkurugenzi mkuu wa tamasha hilo, Dk. Kedmon Mapana, wa Kituo cha Sanaa Chamwino (Chamwino Arts Center-CAC) wandaaji wa tamasha hilo alisema wanatarajia Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, ndiye atakayelifunga rasmi tamasha hilo hiyo kesho.
“Kesho Julai 27, ndiyo tunafikia tamati na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino anatarajia kuwa mgeni rasmi." alisema Dk. Kedmon.
Aidha, alivitaja vikundi vinavyoshiriki tamasha hilo ni pamoja na kutoka Dodoma kuwa ni New Pendo, Yelusalem, Inueni mioyo, Yeriko, Nyota njema, Ushirikiano, Nyerere na Ebenezer.
Vikundi vilivyo vijiji vya Wilaya ya Chamwino ni Upendo (Kijiji cha Dabalo), Imani, Sinai (Kijiji cha Membe). Mchungaji mwema, (Kijiji cha Nzali), Juhudi, Muhubiri (Kijiji cha Kawawa), Nyota njema, Safina, Ndagwa (Kijiji cha Msanga).
Msifuni (Kijiji cha Mlimwa), Nyota, Ufunuo (Kijiji cha Majeleko), Simba (Kijiji cha Mbele zungu) na Inueni mioyo (Kijiji cha Mgunga).
Vikundi kutoka Wilaya ya Kongwa imani ( Kijiji cha Mkutani), Faru (Kijiji cha Songambele) na Safina (Kijiji cha Chigwingili), Pia kikundi cha Uvuke na Upendo (kutoka Manispaa ya Dodoma mjini).
Vikundi vingine ni Mandoo/Tasuba kutoka Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Nazareti (Dar es s Salaam), Muungano (Manyoni, Singida) na Zanzibar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni