Social Icons

Jumanne, 22 Julai 2014

BRAZIL YAMTEUA TENA DUNDA KUCHUKUA MIKOBA YA LUIZ FELIPE SCOLARI


article-0-1FB928EB00000578-209_634x424
Mtu aliyezoeleka: Dunga ameteuliwa kwa mara ya pili kuwa mirthi wa  Luiz Felipe Scolari.
BRAZIL imemtangaza Dunga kwa mara ya pili kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya Luis Felipe Scolari kuachishwa kazi kutokana na kipigo cha mabao 7-1 kwenye mechi ya nusu fainali ya kombe la dunia dhidi ya Ujerumani na 3-0 katika mechi ya mshindi wa tatu na Uholanzi.
Tangazo rasmi limetolewa leo jumanne na sasa kocha huyo mwenye miaka 50 anaanza kazi ya kuwanoa Samba Boys.
Kwa mara ya mwisho Dunda aliyewahi kuwa nahodha wa Brazil mwaka 1994, aliifundisha Brazil katika fainali za mwaka 2010 nchini Afrika kusini na alifukuzwa baada ya kushindwa kufuzu zaidi ya robo fainali.
“Kiukweli nina furaha kubwa kurudi tena,” aliwaambia waandishi wa habari.
Last time: Dunga led Brazil to the quarter-finals at the 2010 World Cup during his previous spell

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates